MAUDHUI NA SIFA ZA WAHUSIKA KATIKA BEMBEA YA MAISHA

MAUDHUI NA SIFA ZA WAHUSIKA KATIKA BEMBEA YA MAISHA SEHEMU YA KWANZA ONYESHA YA 1, 2, 3

  Maudhui ni jumla ya mawazo yote inaozungumzwa katika tamthilia

Katika tamthilia ya bembea ya maisha tunapata maudhui mbalimbali ambao hujitoke katika sehemu tofauti.

 1. Maudhui ya ndoa

Katika sehemu ya kwanza tunapata Yona anaoa Sara na kuishi pamoja

Ndoa ya Yona na Sara imejaa changamoto mbali mbali kama vile kukosa mtoto wa kiume , na vile vile kuteseka kutokana na maradhi ambayo imesababishwa na kuteseka na kuchapwa na mumewe kwa wakati mwingine,

Tunapata Yona anashauriwa kutafuta mtoto wa kiume njee ya ndoa ama kuoa mke mwingine.

Tunapata wasichana wa kisasi pia wanashiriki katika ndoa na kusahau mandugu yao

Neema mtoto wake Sara anashiriki kwa ndoa na Bunju baada ya elimu yake na kuzaa watoto.

 • Maudhui ya utamadani

Mtoto wa kiume huwa kiungo kikubwa sana cha familia kulingana na utamaduni wa jamii za kiafrika.

Tunapata Sara anakosa kujaliwa mtoto wa kiume hali ambayo wanajamii wanaona si sawa hivyo basi wanaanza kumshauri Yona aoe mke wa pili ili amzalie mtoto wa kiume. Aidha anashauriwa kutafuta mtoto wa kiume nje ya ndoa lakini anakataa kushaurika kisa na maana ana msimamo wake na hataki ushawishi wa watu kwenye ndoa yake.    

 • Maudhui ya elimu

Yona na Sara wanaelimisha watoto wao.

Mwanao Neema anafanikiwa kupata kazi nzuri inayomwezesha kujiendeleza kimaisha na vilevile kuweza kugharamia matibabu ya mamake.

Isitoshe,anasalia kuelimisha watoto wake pia.

Anajaliwa mume mzuri pia kutokana na elimu alio nao,hii ni kulingana na Yona .

 • Maudhui ya kazi

Yona na Sara wanapata nafasi ya kuajiriwa kama wafanyi kazi wa nyumbani baada ya  yule mfanyikazi wa kwanza kutoroka kwa kuzidiwa na kazi.

Tunapata kwamba kizazi ya sasa hawawajibiki kazini kisa na maana wanataka kutajirika haraka bila kufanya kazi inavyofaa. Hii ndio sababu ya wengi wao kutoroka kazi.

Sara anafanya kazi kwa bidii  wakati anapolea wanawe.

Neema na mumewe nao wanawajibika katika kazi zao ili kujiendeleza kimaisha.

 • Maudhui ya maradhi

Sara anapatwa na maradhi ambayo yanasababishwa na mateso mengi anayoyapitia mikononi mwa bwanake Yona.

Maradhi haya yanaleta gharama zaidi katika nyumba ya Yona na Sara. Neema anawajibika katika kugharamia matibabu ya mamake.

 • Nafasi ya mwanamke katika jamii

Sara anafanya kazi kwa bidii ili aelimishe watoto wake. Aidha anavumilia mateso mengi anayoyapitia ili kusimamisha ndoa yake isije ikasambaratika.

Neema anapata elimu bora,anakuwa msomi, mwenye bidii na anayewajibika kusomesha wanae na kugharamia matibabu ya mamake.

 • Nafasi ya watoto katika ndoa

Watoto huonekana kuwa muhimu sana katika ndoa. Na mara nyingi jamii huonea fahari mtoto wa kiume. Katika tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ tunaona mtoto kama mwokozi. Neema ambaye ni mtoto wa sara anagharamia matibabu ya mamake anapougua kutokana na dhulma.

SIFA ZA WAHUSIKA

 1. YONA
 2. Mbabe dume/mwenye taasubi ya kiume

Yona hakuweza kumsaidia Sara katika kufanya kazi za nyumbani. Aidha alimdhulumu sana mke wake hadi akawa mgonjwa.

 • Mwajibikaji

Yona anawajibika katika kusomesha watoto wake

 • mkatili

Anamchapa na kumtesa mkewe hadi anaugua

 • Ana msimamo dhabiti

Anakataa kutafuta mtoto wa kiume nje ya ndoa. Pia anakataa kukubali ushawishi wa kuoa mke wa pili ili amzalie mtoto wa kiume.

 • mtamaduni

anaamini mtoto wa kwanza hana budi kumsaidia mzazi.

 • Mlevi

Yona alianza kulewa kisha kumchapa mkewe.

 • Mkosa shukrani

Yona anakosa kuona mchango wa mwanawe Neema hata baada ya kumpeleka Sara hospitalini.anaona kwamba anafaa kufanya zaidi ya yale ambayo tayari amefanya.

 • Mwenye tuhuma

Anaamini kwamba Sara anamsema na watoto wake

 • SARA
 • Mvumilivu

Sara anavumilia mateso ya kuchapwa na mumewe.

Aidha anakabiliana na changamoto mengi yanayokabili ndoa yake lakini anayavumilia ili familia yake isisambaratike.

 • Mwenye bidii

Wakati alikuwa na afya njema hakuwahi kosa kufanya kazi zake.

Aidha anasaidiana na mumewe kufanya kazi ili kuwasomesha watoto wao.

 • Mwajibikaji

anawajibika kazini ili kusomesha watoto wake

 • mwenye shukrani

Tofauti na Yona ,Sara anaona mchango wa Neema katika kumgharamia kimatibabu anapougua.

 • Rafiki wa dhati

Ni rafiki wa karibu sana wa Dina

 • NEEMA
 • Msomi

Anapata elimu bora inayomwezesha kupata kazi nzuri

 • Mwajibikaji

Anawajibika kazini na kuhakikisha kuwa mamake amepata matibabu mazuri anapougua.

 • Mkarimu/mwenye utu/mwenye huruma

Anajitolea kugharamia matibabu ya mamake na hata kulipa karo ya Kiwa.

 • Mwenye akili pevu

Anafaulu katika masomo yake na kisha baadaye anajaliwa kupata kazi.

 • DINA
 • Rafiki wa dhati

Ni rafiki wa karibu sana wa Sara.

Anamsaidia kufanya kazi za nyumba anapougua.

 • Mcha Mungu

Mambo yake mengi anarejelea Mungu,anasema kwamba Mungu ni mkuu.

 • Mlezi mwema

Anashangaa kwa nini Kiwa hali vizuri, anataka awe na misuli.

 • Mwenye busara

Anampa Kiwa kauli ya busara kuhusu maisha.

 • Mshauri mwema

Anamshauri Sara kutofikiri sana mambo ya watu wengine bali ashukuru kwamba hata akiwa mgonjwa anapata msaada kutoka kwa mwanawe.

 • KIWA
 • Ni kijana wa sasa

Amezinduka na anaelewa kuwa dunia ya sasa haithamini kimo au kutetemeka kwa misuli bali inathamini akili pevu.

 • Mwajibikaji

Anawajibika kurudi nyumbani kumwona mamake.

 • BUNJU
 • Msomi

Anasoma kisha kupata kazi baadaye na kumnunulia mkewe gari.

 • Mwajibikaji

Anapofanya kazi anahakikisha kwamba ametekeleza majukumu yote nyumbani kwake hivi kwamba pesa zake mkewe amemwachia atumie anavyotaka.

 • Mwenye mapenzi ya dhati

Anamnunulia mkewe gari,hii ni njia mojawapo ya kuonyesha mapenzi

Print Friendly, PDF & Email
people found this article helpful. What about you?

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x