KCPE PAST PAPERS 2011 KISWAHILI LUGHA QUESTION PAPER

 Manyam Franchised Tests

KISWAHILI   |   KCPE   |   2011

 


NAME…………..……………..…………. SCHOOL…………….…………………DATE……………… TIME: 2 hours


Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa

            Wakati wa vitongoji duni ___1___ na matatizo mengi. Asilimia kubwa ya waja hapa ___2___ ___3___ aila. ___4___, katika mitaa ya mabwanyenye ___5___ na vitongoji hivi, hali ni tofauti;

Majumba yenye kuvutia yamepamba mazingira humo. Maisha ya makundi haya mawili ___6___. Wana wa matajiri hupata mahitaji ___7___ huku maskini __8___ kwa ukosefu. Ama kwa kweli ___9___

            A                                 B                                  C                                  D

  1. Wametwaliwa               wamekabidhiwa wametengwa                 wametingwa
  2. Haiwezi                        hawawezi                      haziwezi                       hamuwezi
  3. Kumkimu                     kuzikimu                      kujikikmu                     kuwakimu
  4. Labda                           kwa hivyo                     hata hivyo                     ingawa
  5. Waliyopakana               iliyopakana                   uliyopakana                  yaliyopakana
  6. Yamebaidika kama        yameadimika kama        yameingia kati kama      yamejikaukia kama

ardhi na mbingu            kama wali wa daku        mchuzi wa ugali            ukuni

  1. Zote                             yote                              nyote                            sote
  2. Wakila mwata               wakila mwande             wakila yamini               wakila hasara
  3. Dua la kuku halimpati    bidii ya mja haiondoi     duaa mnyonge               mtegemea mundu

Mwewe                        kudura                          haliendi joshi                haachi kunona

Tina alijua kwamba alihitaji kutia bidiii masomoni asije ___10___ shule. Kijijinni mwao ilikuwa kawaida wasichana ___11___ nafasi katika elimu. Palipotokea uhaba ___12___ karo, masomo ya msichana ___13___ huku mvulana akiendelea na elimu. Mara hii Tina aliamua kutia bidii ili angaa Mwalimu Mkuu amtafutie mhisani ___14___. Kwa njia hii Tina ___15__ namna ya kuliokoa tabaka lake.

            A                                 B                                  C                                  D

  1.  Akaachishwa                            akaachiwa                     akaachilia                     akaachia
  2. Kunyanyaswa                            kubadilishiwa                kudhulumiwa                kupunguzwa
  3. Ya                                            kwa                              wa                                na
  4. Yangekatizwa                           yanakatizwa                  yakikatizwa                   yakakatizwa
  5. Ayathamini masomo yake          amthamini masomo       amdhamini masomo       ayadhamini masomo yake

yake                             yake

  1. Alitarajia alipata                        alijihimu alipata            alijihimu kupata            alitarajia kupata


Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu lililo sahihi

  1. Sentensi inayounganisha sentensi: “Juma ni mzee. Juma anasoma kitabu bila miwani.” Kisahihi ni:

A.    Juma ni mzee maadamu anasoma kitabu bila miwani

B.     Juma anasoma kitabu bila miwani licha ya kuwa yeye ni mzee

C.     Juma ni mzee madhali anasoma kitabu bila miwani

D.    Juma anasom kitabu bila miwani minghairi ya yeye ni mzee

  1. Ki katika sentensi, “Mwanafunzi huyo akikuona atatembea kijeshi,” imetumiwa kuonyesha;

A.    Masharti, nomino

B.     Wakati, nomino

C.     Masharti, namna

D.    Wakati, namna

  1. Chagua neno ambalo limetumia silabi changamano

A.    Mbuga

B.     Kituta

C.     Ziwa

D.    Utulivu

  1. Kamilisha, ‘Fahamika kama___

A.    Sahani na kawa

B.     Kinu na mchi

C.     Pua na mdomo

D.    Tui na maziwa

  1. Chagua sentensi yenye vivumishi

A.    Mwashi amejenga nyumba juu ya mlima

B.     Yule aliimba vizuri mno akatuzwa

C.     Nokoa atafika hapa hivi punde

D.    Wanafunzi wengi walifaulu mtihani huo

  1. Ni sentensi ipi ambayo imetumia ‘kwa’ kuonyesha sehemu ya kitu

A.    Alitembea moja kwa moja hadi shuleni

B.     Wazee kwa vijana walihudhuria sherehe hiyo

C.     Watu watatu kwa kumi huepuka mitego

D.    Monika alipongezwa kwa wazazi wake

  1. Mkono wazi ni kwa ukarimu ilhali_____ni kwa inda

A.    Jicho la nje

B.     Joka la mdimu

C.     Kifauongo

D.    Kisebusebu

  1. Chagua kifaa cha uhunzi

A.    Fuawe

B.     Patasi

C.     Timazi

D.    Chetezo

  1. Ni kundi lipi lenye sauti ghuna pekee?

A.    P, t,  z

B.     V,  th,  n

C.     Sh,  l,  w

D.    B,  d,  g

  1. Wingi wa, ‘Kiduka hicho kilifunguliwa jana.’ Ni:

A.    Maduka hizo zilifunguliwa jana

B.     Viduka hizo zilifunguliwa jana

C.     Viduka hivyo vilifunguliwa jana

D.    Maduka hayo yalifunguliwa jana

  1. Ni sentensi ipi sahihi?

A.    Hewala! Nitakusaidia

B.     Kefule! Naomba maji

C.     Oyee! Tumeshindwa

D.    Hamadi! Amekuja

  1. Miaka mia ni kwa karne ilhali vitu ishirini ni kwa

A.    Kikwi

B.     Korija

C.     Mwongo

D.    Lukuki

  1. Chagua sentensi yenye kiwakilishi cha idadi

A.    Mwanafunzi aliyefika kwanza alimpata mwalimu wa pili darasani

B.     Mwalimu aliyetufunza mwanzoni alituuliza swali moja mara mbili

C.     Mwalimu aliyetufunzamwanzoni alitufafanulia mambo kadha ya kutufaa

D.    Mwanafunzi aliyefika kwanza alipewa medali na wa pili akapewa kitabu

  1. Ni sentensi ipi ambayo imetumia sitiari?

A.    Mwakio ni sungura siku hizi

B.     Moyo wake ulimwambia asirudi nyuma

C.     Muuguzi alisema atajifungua salama

D.    Nyaboke ni mpole kama njiwa

  1. Ikiwa juzi ilikuwa Jumatatu, jumamosi itakuwa;

A.    Kesho

B.     Mtondo

C.     Mtondogoo

D.    Kesho kutwa


Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31-40

Mfumo wa elimu nchini unatilia mkazo mafunzo mengine ambayo, japo yamo nje ya masomo ya kawaida, yanahusiana na kwenda sambamba na masomo hayo ya kawaida. Vyama vya wanafunzi shuleni vinachangia pakubwa kupitisha mafunzo hayo ya ziada.

Vyama vya wanafunzi hutofautiana kulingana na majukumu. Mathalani, vipo vyama vya kidini, vya kitaaluma na vya michezo. Pia, kuna vyama vya kijamii kama vile chama cha kupambana na matumizi mabaya ya dawa na vya kiuchumi kama vile chama cha wakulima chipukizi.

Imedhihirika kwamba vyama vya wanafunzi vina manufaa ya kuhusudiwa. Hii ndiyo sababu shuleni, kila mwanafunzi anahimizwa kujiunga na angaa vyama viwili. Vyama vya wanafunzi huwasaidia kukuza vipawa na kuimarisha stadi za kujieleza. Haya hufikiwa kupitia kwa shughuli za vyama kama vile ukariri wa mashairi, mijadala, uteguaji vitendawili, chemsha bongo na ulumbi. Aidha, vyama hivi huhimiza utangamano miongoni mwa wanachama kwani wao hujiona kuwa watu wenye mwelekeo mmoja. Vilevile utangamano wa kitaifa na kimataifa hujengeka.

Mwanafunzi ambaye amejiunga na vyama vya wanafunzi huweza kukabiliana na changamoto za maisha kwa urahisi kuliko yule ambaye hajawahi kujiunga na chama chochote. Katika vyama hivi, wanafunzi hufunzana mikakati na maarifa ya kutatua matatizo na mbinu za kuepuka mitego ya ujana. Kupitia kwa ushauri wa marika kwa mfano, mwanafunzi hushauriwa kuhusu masuala kama vile uteuzi wa marafiki, kuratibu muda, kujikubali na kuwakubali wenzake.

Hali kadhalika, mwanafunzi hujifunza maadili ya kijamii na kidini. Kupitia kwa vyama vya kidini na vinginevyo, yeye hujifunza kujistahi na kuwa stahamala ya kidini, kitikadi na kikabila. Kadhalika, majukumu ambayo mwanafunzi huenda akapewa hupalilia uwajibikaji, uaminifu na kipawa cha uongozi. Hata anapohitimu masomo yake, mwanafunzi huyu huendeleza sifa hizi.

Vijana wana nafasi kubwa katika kukabiliana na maovu ya kijamii kwani wao ndio wengi zaidi. Kupitia kwa vyama hivi, wanafunzi wanaweza kuwahamasisha wenzao dhidi ya tabia hasi kama vile kushiriki mapenzi kiholela, ulanguzi wa dawa za kulevya na kujiingiza katika burudani zisizofaa. Pia, shughuli na miradi ya vyama hivi huwawezesha wanafunzi kutumia nishati zao kwa njia ya kujinufaisha na kuepuka maovu. Kwa mfano, wanaweza kwenda kukwea milima, kufanya matembezi ya kukusanya pesa za kuwafadhili wahitaji, kuendeleza shughuli za kunadhifisha mazingira na kutembelea vituo vya mayatima na wazee.

Kushiriki katika vyama vya michezo hakumwezeshi mwanafunzi kuimarisha afya na kujenga misuli tu, bali pia huweza kuwa msingi wa kupata chanzo cha riziki baadaye. Wapo wachezaji maarufu ambao walitambua na kuviendeleza vipawa vyao kupitia kwa vyama vya aina hii, ha hivi sasa wana uwezo wa kuyaendesha maisha yao na familia zao.

Ifahamike kuwa vyama vya wanafunzi vinapaswa kuwa msingi wa mashikamano na maridhiano. Visitumiwe kama vyombo vya kuwagawa wanafunzi kitabaka. Mwanafunzi hana budi kusawazisha muda anaotumia. Atenge muda wa shughuli za vyama na kudurusu masomo yake.


  1. Kulingana na kifungu, mwanafunzi akiwa shuleni

A.    Hufunzwa mfumo sambamba, hufunzwa kupitisha mafunzo ya ziada

B.     Hujiunga na vyama, hujifunza mfumo sambamba

C.     Hufunzwa mfumo sambamba, hufunzwa taaluma ya vyama

D.    Hujiunga na vyama, hujifunza taaluma mbalimbali

  1. Katika aya ya pili, wazo kuu analozungumzia mwandishi ni;

A.    Aina za vyama vya kijamii

B.     Majukumu ya vyama vya wanafunzi

C.     Aina za vyama vya wanafunzi

D.    Majukumu ya vyama vya kijamii

  1. Chagua jibu lisilo sahihi kwa mujibu wa taarifa

A.    Vyama vya wanafunzi huchangia kukuza ubunifu wa wanafunzi

B.     Vyama vya wanafunzi huchangia kukuza uzalendo wa kimataifa

C.     Vyama vya wanafunzi huwasaidia kuimarisha uzalendo na mahusiano mema

D.    Vyama vya wanafunzi huwasaidia kuimarisha uhusiano na nchi nyingine

  1. Kifungu kinaonyesha kuwa ushauri na uelekezaji

A.    Humwezesha mwanafunzi kujithamini

B.     Humsaidia mwanafunzi kupata marafiki

C.     Humwandalia mwanafunzi mpangilio wa kazi

D.    Humwondolea mwanafunzi mitego

  1. Kwa mujibu wa taarifa, jibu linalodhihirisha maana ya methali, “Ukiona vyaelea vimeundwa,” ni

A.    Wanafunzi wakipewa nafasi ya uongozi huheshimu mielekeo ya wengine

B.     Wanafunzi wakipewa nafasi ya uongozi hujistahiki na kustahimili wengine

C.     Wanafunzi wakipewa nafasi ya uongozi huhimiza stahamala ya kidini baadaye

D.    Wanafunzi wakipewa nafasi ya uongozi huwa wa kutegemewa baadaye

  1. Kulingana na kifungu, vijana wanaweza kudhihirisha uwajibikaji katika jamii kupitia

A.    Kuwapinga walanguzi wa dawa za kulevya na kuepuka burudani.

B.     Kufanya matembezi anuwai ya kukusanya pesa

C.     Kushiriki katika miradi ya kuwaauni wanyonge

D.       Kuendeleza shughli za kuhifadhi mazingira na kutembea milimani

  1. Kifungu kimebainisha kuwa:

A.    Vijana ndio wanaoweza kushiriki mapenzi kiholela

B.     Vijana wanaweza kutumiwa kama msingi wa kustawisha vituo vya wahitaji.

C.     Vijana wanaweza kutumiwa kama msingi wa kuadilisha jamii pana.

D.     Vijana ndio wanaoweza kukabiliana na matatizo ya kijamii.

  1. Chagua jibu sahihi kulingana na kifungu.

A.    Michezo huweza kumjengea mtu jina na kumwimarisha kiuchumi.

B.     Wachezaji maarufu walianza kucheza walipojiunga na vyama

C.     Wachezaji maarufu walianza kugundua vipawa vyao walipojiunga na vyama

D.    Michezo huweza kumjengea mtu uwezo na kumwimarisa kiuchumi.

  1. Maoni ya mwandishi katika aya ya mwisho ni kwamba:

A.    Vyama vya wanafunzi vinaweza kuvurungu usawa katika jamii.

B.     Vyama vya wanafunzi ndio msingi wa kumsaidia mwanafunzi kutumia muda wake darasani.

C.     Vyama vya wanafunzi vinaweza kuvurunga masomo katika darasa.

D.      Vyama vya wanafunzi ndio msingi wa kuimarisha umoja na maelewano katika jamii.

  1. Kulingana na kifungu, ‘manufaa ya kuhusudiwa’ ni:

A.    Manufaa yanayowafaidi wengi

B.     Manufaa yanayowavutia wengi

C.     Manufaa yasiyosahaulika kwa urahisi

D.    Manufaa yasiyopatikana kwa urahisi.

 


Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 mpaka 50

Naikumbuka siku hiyo vizuri. Niliamka alfajiri mbichi tayari kuanza safari kutoka kijiji mwetu hadi Mji Mkuu. Hii ndiyo iliyokuwa mara yangu ya kwanza kuuzuru mji huu. Moyoni nilikuwa na bashasha isiyokuwa ya kawaida kwa sababu siku hiyo ningeuona mji ambao sifa zake nilikuwa nikizisikia tu kutoka kwa wenzangu waliobahatika kuutembelea. Hamu ya kuona majengo marefu, barabara zilizosakifiwa, magari mengi, watu wa aili mbalimbali na mabustani ya starehe ilinigubika, nikawa sijifai kwa matumaini.

 

Nilitembea hatua chache hadi kituo cha mabasi, nikapata daladala moja iliyotoza nauli nafuu, nikaiabiria mpaka mji uliokuwa pua na mdomo kutoka kitongojini mwetu. Hapo nilitumainia kupata matwana ya kusafiria hadi mji mkuu. Kwenye stesheni kulikuwa na msongamano wa matwana na harakati za utingo waliokuwa waking’ang’ania abiria. Nikaingia katika matwana moja iliyoitwa Upepo. Nilikuwa abiria wa kumi na mbili kuingia. Baada ya dakika tano hivi, gari lilijaa abiria, wote kumi na wanne. Tukang’oa nanga. Mandhari ya kupendeza yalijikunjua mbele yangu. Upepo mwanana kupitia dirishani, mpito wa kasi wa miti, mazigazi… vyote vilishirikiana kunipumbaza kiasi cha kunisahaulisha kufunga mkanda wa usalama.

Baada ya robo saa, utingo alidai nauli. Nikapeleka mkono kwa tahadhari kwenye kibindo changu ambamo nilikuwa nimezifutika hela za usafiri na masurufu. Nikatoa noti ya shillingi mia mbili na kumkabidhi utingo huku nikitarajia baki. Utingo alinikazia macho, akanyoosha mkono na kusema, “Mia zaidi!” nikarudi tena kwenye kibindo, nikatoa noti mbili za shilingi hamsini na kumpa. Safari ikaendelea.

 

Tulipofika mji mdogo wa Pitia, matwana ilisimama. Utingo aliinama chini ya viti, akatoa vibao na kuviweka baina ya viti vya kawaida. Kisha akaanza kutangaza, “Wa jiji na mia; mia hamsini,” Abiria walionekana kuwa wachovu kwa kungojea na kupigwa na mzizimo wa kipupwe walipigana vikumbo kuingia, huku utingo akiwaelekeza kwenye vile vibao. Viti vilivyotengenezewa abiria watatu vikaishia kubeba abiria watano! Matwana nayo ikawa haina budi kustahimili uzito wa abiria ishirini  na watatu. Tukawa tunabanana kweli kweli. Utingo naye alining’inia mlangoni, shati lake lapeperushwa na upepo. Nilipojaribu kulalamika hali hii nilinyamazishwa hata na abiria wenzangu.

Gari likaanza mwendo tena huku likiendeshwa kwa kasi ya umeme. Abiria waliokuwa wakizungumza sasa walinyamaza, kila mmoja roho I mkononi. Kimya cha kaburi kikatawala hadi pale utingo alipomwambia dereva, “Weka ngoma,” Muziki ukahanikiza hewani kwa fujo. Baadhi ya abiria wakaanza kuyumbisha vichwa kwa kufuata mdundo wa muziki ambao ulitishia kuvipasua viwambo vya maskio yangu.

 

Njiani tulikutana na walinda usalama ambao walitusimamisha. Utingo alishuka na kwenda chemba na mmojawapo wa hao maafisa, kisha akarudi huku kipaji chake kimenawiri kwa tabasamu. Akasema, “Nimempaka mafuta viganjani.” Baadhi ya abiria walitikisa vichwa, wengine wakacheka kama kwamba wameona kinyago. Mimi nilibaki kuduwaa tu. Gari liliongeza mwendo na baada ya muda mfupi tukafika kwenye mji mmoja ambao ulikuwa ma majengo makubwa makubwa. Nikadhani tumefika mji mkuu. Nilipomuuliza abiria jirani aliniambia kuwa huu ulikuwa tu mji mkuu wa jimbo la Buraha. Tukazidi kuyakunja masafa ya safari hii kwa kasi ya kuogofya huku dereva akitafuna majani aliyokuwa akiyatoa mfukoni mwa shati lake. Kadiri alivyoyatafuna ndivyo alivyzidisha kasi. Nikahisi kama gari linapaa juu angani. Nikataka kumwambia dereva jambo, lakini nikajiasa, “ikiwa wengine wamenyamaza sembuse mimi?”

Baada ya kitambo kidogo mvua ilianza kunyesha. Kukawa na ukungu na utelezi barabarani. Abiria mmoja alimsihi dereva kupunguza mwendo. Haya hayakumgusa dereva mshipa. Aliongeza kasi kana kwamba hajaskia lolote. Gari lilifika kwenye kuruba, dereva akawa haoni vizuri. Ghafla nikaskia,”Kirr…!” kisha “Mungu wangu!” halafu, “Ngu!”

Kiza cha kaniki kikatanda


  1. Kulingana na kifungu

A.    Wenzake msimulizi waliwahi kupata fursa ya kuishi katika Mji Mkuu

B.     Barabara za mji mkuu hazina mashimo

C.     Mji mkuu ana majumba mengi marefu

D.    Msimulizi ana mwao na hali ilivyo katika mji mkuu

  1. Chagua jibu sahihi kuhusu vituo vya magari kwa mujibu wa aya ya pili

A.    Wasafiri wengi kushindania nafasi

B.     Magari mengi kushindania wasafiri

C.     Misongamano mingi ya kutangazia wasafiri

D.    Shughuli nyingi za kunadia nafasi

  1. Mazingira ya kuvutia yalimwathiri msimulizi kwani

A.    Aliduwaa na kujisahau

B.     Alifurahia upepo na kujisahau

C.     Alizubaa na kupuuza sheria za usafiri

D.    Alipumbaa na kupinga sheria za usafiri

  1. Msimulizi alikuwa amehifadhi pesa katika

A.    Mfuko mdogo ndani ya suruali

B.     Mfuko mdogo mbele ya suruali

C.     Mkunjo wa nguo iliyoshonwa kiunoni

D.    Mkunjo wa nguo uliofungwa kiunoni

  1. Katika mji wa Pitia abiria walipigana vikumbo kuingia garini kwa sababu

A.    Kulikuwa na uhaba wa magari

B.     Kulikuwa na uhaba wa viti

C.     Walikuwa wamechoka kungojea matwana upepo

D.    Walikuwa wamepigwa na baridi na mvua

  1. Kulingana na kifungu, ajali barabarani husababishwa na

A.    Ukosefu wa magari, kubeba abiria wengi

B.     Kiburi cha madereva, kutozingatia maelekezo barabarani

C.     Ukosefu wa mikanda ya usalama, madereva kutowajibika

D.    Muziki wa kupasua viwambo, madereva kutoona vizuri

  1. Msimulizi ni mkakamavu kwa vile

A.    Alishutumu hali ya gari kubeba abiria kuliko kiasi

B.     Alishutumu hali ya shati na utingo kuning’inia nje

C.     Alinyamaza alipoona dereva akikaribia kuruba kwa kasi

D.    Alinyamaza alipoona utingo akienda chemba na afisa

  1. Chagua jibu lisilo sahihi kulingana na kifungu

A.    Abiria wengine walifurahia muziki garini

B.     Ufisadi unaweza kusababisha ajali barabarani

C.     Abiria wanaweza kuzuia ajali barabarani

D.    Kuruba ndiyo iliyosababisha ajali garini

  1. Ni mfuatano upi wa matukio ufaao kwa mujibu wa kifungu?

A.    Kucheza muziki, kukutana na polisi, kufikia kuruba, mvua kunyesha, kupata ajali

B.     Kukutana na polisi, kuhonga, kucheza muziki, kufikia kuruba, kupata ajali

C.     Kucheza muziki, kukutana na polisi, kuhonga, kufikia kuruba, kupata ajali

D.    Kukutana na polisi, gari kupaa juu, mvua kunyesha, kufikia kuruba, kupata ajali

  1. ‘Kiza cha kaniki kikatanda.’ Kulingana na kifungu ina maana

A.    Msimulizi alopoteza fahamu

B.     Msimulizi akapoteza uwezo wa kuona

C.     Kukawa na weusi mkubwa

D.    Kukawa na giza totoro

 

KCPE PAST PAPERS 2011 KISWAHILI LUGHA QUESTION PAPER

icon envelope tick round orange animated no repeat v1 Virus-free.www.avast.com

Print Friendly, PDF & Email
people found this article helpful. What about you?

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x