KCPE PAST PAPERS 2006 KISWAHILI LUGHA MASWALI NA MAJIBU

2006 ANSWERS 1

 Manyam Franchised Tests

KISWAHILI   |   KCPE   |   2006

 

NAME…………..……………..…………. SCHOOL…………….…………………DATE……………… TIME: 2 hours


Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

            Kandamiza hakujua thamani ___1___ watoto ___2___ siku moja ___3___ na ulimwengu. Alizoea kuwatumikisha watoto wadogo kwa ___4___ kuwaajiri watu wazima asije akajiumiza kwa kuwalipa mishahara mikubwa. Siku moja mwanawe mmoja ambaye ___5___ kuyamudu masomo aliamua kuondoka nyumbani bila kuaga. Kandamiza alipogundua kuwa mwanawe ___6___ mjini aluhuzunika mno. Moyoni Kandamiza alijua kuwa mtoto huyo ___7___ jinsi yeye alivyowafanya watoto wa wengine.

            A                                  B                                  C                                  D

  1. Wa                               la                                  za                                 ya
  2. Sasa                             hadi                              tangu                            lau
  3. Alipofunzwa                  alikofunzwa                   aliofunzwa                    aliyefunzwa
  4. Kuchelewa                    kupenda                        kucheka                        kupendelea
  5. Hawezi                         hakuweza                      hataweza                       hajaweza
  6. Ametoroka                    ametoroshwa                 ametorokea                   ametorosha
  7. Angetesa                       angemtesa                     angewatesa                    angeteswa

Taifa lolote___8___ wananchi wenye afya. Magonjwa ___9___ nchi hasara ___10___ pia huwa mzigo mzito kwa mtu binafsi. ___12___ ya magonjwa hutokana na___13___usafi. ___14___ huweza kuzuiwa iwapo wananchi wataitikia wito wa kunadhifisha makazi ___15___

            A                                  B                                  C                                  D

  1. Huhitaji             hahitaji                          yahitaji                          lihitaji
  2. Hailetei                         haileti                            hayaleti                         hayailetei
  3. Ajabu                           kamwe                          tu                                 naam
  4. Bali                              mbali                            na                                 ijapokuwa
  5. Baina                            baadhi                           kati                               zaidi
  6. Kutodumisha                 kutodumu                     kudumisha                    kudumu
  7. Hii                                hizi                               hiyo                              haya
  8. Lao                              yao                               zao                               wao

 

 


Kutoka swali la 16 mpaka 30 chagua jibu lililo sahihi

  1. “Ki” imetumiwaje katika sentensi: Mweni alipokuja alinipata nikifyeka

A.     Kuonyesha hali ya masharti

B.     Kuonyesha hali ya kukanusha

C.     Kuonyesha hali ya kuendelea

D.    Kuonyesha hali ya udogo

  1. Ni sentensi ipi sahihi?

A.     Ndizi lililoletwa ni langu

B.     Miti zilizopandwa zimeota

C.     Zulia iliyonunuliwa ni zuri

D.    Wema unaozungumziwa ni huu

  1. Miongoni mwa sehemu hizi za mwili, ni sehemu ipi iliyo tofauti na zingine?

A.     Paja

B.     Kiganja

C.     Pafu

D.    Goti

  1. Polepole, vibaya, alasiri, njiani, ni

A.     Vielezi

B.     Vivumishi

C.     Nomino

D.    Viwakilishi

  1. Methali inayotoa funzo kuwa: jambo linaloonekana zito kwa mwingine laweza kuwa rahisi kwako ni;

A.     Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi

B.     Mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi

C.     Kila mwamba ngoma ngozi huvutia kwake

D.    Ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno

  1. Sentensi “Asingalikwenda kwake asubuhi ansingalimkuta” ina maana kuwa;

A.     Hakuenda kwake asubuhi lakini alimkuta

B.     Alienda kwake asubuhi lakini hakumkuta

C.     Alienda kwake asubuhi na akamkuta

D.    Hakuenda kwake asubuhi wala hakumkuta

  1. Ni maneno yapi ambayo yote ni viunganishi?

A.     Ila, ingawa, lakini, maadamu

B.     Huyu, hao, ovyo, na

C.     Ila, lakini, vizuri, wima

D.    Ingawa, isipokuwa, zuri, safi

  1. Kivumishi cha sifa kutokana na kitenzi angaa ni:

A.     Angaza

B.     Angazia

C.     Angavu

D.    Angalau

  1.  kwa maneno ni:

A.     Subui nane

B.     Thumuni saba

C.     Subui

D.    Thumuni

  1. Kisawe cha neno barobaro ni

A.     Banati

B.     Kijana

C.     Mvulana

D.    Shaibu

  1. Nomino habari iko katika ngeli ya:

A.     U-ZI

B.     I-I

C.     U-I

D.    I-ZI

  1. Tano ni kwa chokaa. Kitita ni kwa

A.     Pesa

B.     Funguo

C.     Ndizi

D.    Ngozi

  1. Haya ni maumbo gani?

A.   Pembe tatu, Mche, Duara

B.    Pia, Mcheduara, Nusuduara

C.   Pia, Mchemramba, Mcheduara

D.   Pembe tatu, Pia, Nusuduara

  1. Chagua usemi halisi ufaao wa:

Bahati alisema kuwa angeenda nyumbani kupumzika

A.     “Nimeenda nyumbani kupumzika,” Bahati alisema

B.     “Niende nyumbani kupumzika,” Bahati alisema

C.     “Nitaenda nyumbani kupumzika,” Bahati alisema

D.    “Nilienda nyumbani kupumzika,” Bahati alisema

  1. Yapange maneno yafuatayo kulingana na jinsi yanavyotokea katika kamusi:

(i)               Bandika

(ii)              Beua

(iii)            Birika

(iv)            Baidika

A.     (i) (iv) (ii) (iii)

B.     (iv) (ii) (iii) (i)

C.     (ii) (i) (iii) (iv)

D.    (iv) (i) (ii) (iii)


Soma taarifa hii kisha ujibu maswali 31 mpaka 40

      Huko Tujueni aliishi mtu kwa jina Mkazeni. Mkazeni alikuwa maarufu katika kutabiri ndoto. Alijulikana pia kwa kuyadadisi mambo yaliyozuka humo kijijini mwao. Kwake kulifurika watu ambao aliwahudumua bila malipo.

      Wakati fulani Mkazeni alioteshwa kuwa kulikuwa na magari na matrela ambayo yalikuwa yakisimamishwa humo kijijini. Madereva wake walikuwa watu waliojaa wadudu tele mwilini. Madereva hao walikuwa wakiwalaghai vijana kijijini huku wakiwaachia “zawadi” zilizileta “vilio”. Alipowaeleza wanakijiji wakamcheka na kumwambia, “sasa nguvu zako za utabiri zinapotea . utawezaje kufikiria kuwa magari hayo yataleta balaa? Magari hubebea mali!”

      Ingawa maneno hayo yalisemwa kiutaniutani, yalimchoma maini, akaamua kufyata ulimi na kukaza nia yake. Alijitahidi kuihimiza aila yake kuhusu umuhimu wa tabia njema.

      Siku nyingine tena akaota ndoto kuwa huko Tujueni kumeingia joka kubwa lililowameza vijana wengi.Ingawa wanakijiji walikuwa wamepuuza hapo awali; aliwafafanulia ndoto hiyo nao wakazidi kumcheka. “Sasa tena utabiri umeleta mambo ya nyoka? Tangu uzaliwe umewahi kumwona nyoka kama huyo?” hapo Mkazeni akaona amedharauliwa kupita kiasi, akaamua “kujimezea” utabiri wake mwenyewe, lake liwe jicho tu. Watu ambao waliamua kutojihadhari kabla ya hatari, angewafanya nini? Kidole kimoja kingevunjaje chawa?

      Miaka michache ikapita, nayo magari na matrela ya kikweli yakafika pale na kupafanya kituo cha mapumziko. Madereva wakaiona sehemu hiyo ikiwa na starehe nyingi. Tujueni ikajulikana. Bishara madukani na kwenye masoko zikaongezeka.

      Baadhi ya watu waliokuwa wamepuuza Mkazeni wakasema, “Oneni mtabiri yule na ndoto zake. Maafa aliyoyatabiri ni hizi pesa tunazozipata? Alitaka tufe maskini? Muone sasa, amenyamaza jii kama maji ya mtungi. Anasema anaihubiria familia yake isijihusishe na biashara haramu. Biashara gani haramu hapa? Cha kupata si cha kuiba.”

      Baada ya muda, familia nyingi zikaanza kulia. Utabiri ukaja kutokea kweli. Wadudu walikuwa ni UKIMWI na joka likawa maangamizi yaliyoletwa na madhara ya UKIMWIA. Wanakijiji waliathirika na kujuta. Kituo hicho cha biashara kikawa na sifa mbaya. Watu wengi wakafa na biashara ikazidi kufifia.

      Mkazeni akawa anasikitishwa na matokeo ya mapuuza na tamaa za wanadamu. Kwake yeye na familia yake waliendelea kuishi vyema kinidhamu.


  1. Mkazeni alikuwa karimu kwa sababu

A.     Alitabiri mambo mengi bila chuki

B.     Aliwatabiria watu mambo bila kuwalipisha

C.     Watu wengi walimwendea kwa utabiri

D.    Watu wengi walimdharau lakini hakulipiza

  1. UKIMWI ndotoni unaweza kulinganishwa na

A.     Wadudu na joka kubwa

B.     Matrela na madereva

C.     Madereva wenye wadudu

  1. Wanakijiji wanaposema, “Sasa nguvu zako za utabiri zinapotea” wanamaanisha

A.     Mkazeni si mtabiri tena

B.     Wanaushuku utabiri wa mkazeni

C.     Hawautaki utabiri wa Mkazeni

D.    Mkazeni hutabiri yasiyo ya kweli

  1. Bishara madukani ziliongezeka kwa sababu

A.     Watu wengi walikuja kutafuta utabiri wa Mkazeni

B.     Kulikuwa na starehe nyingi katika masoko

C.     Tujueni ilikuwa kituo cha mapumziko cha madereva wa matrela

D.    Tujueni ilijulikana na madereva wa matrela makubwa

  1. Watu wengi wa tujueni walikuwa ni

A.     Wenye tamaa na watabiri

B.     Wapuuzaji na watabiri

C.     Wenye tamaa na malezi bora

D.    Wapuuzaji na wenye tamaa

  1. Kulingana na taarifa hii, UKIMWI uliendelezwa sana na:

A.     Madereva wa magari na matrela

B.     Wafanyibiashara wenye matrela na magari

C.     Madereva wapitiao katika vituo vya biashara

D.    Wazazi wenye tamaa ya kupata mali

  1. Baada ya Mkazeni kupuuzwa tena alichukua hatua zipi?

A.     Alitabiri mara ya pili na kungojea matokeo

B.     Alibishana na wapuuzaji na kuwapa matokeo

C.     Aliwaangalia tu waliompuuza na kuendelea kutabiri

D.    Alinyamaza, akaongoza familia na kungoja matokeo

  1. Kutojihadhari kabla ya hatari ni sawa na:
  1. Kutojitayarisha kukabiliana na tatizo
  2. Kutoshughulika na hatari
  3. Kutoshughulikia matatizo yajapo
  4. Kutoogopa madhara ya tatizo
  1. Familia ya Mkazeni ilinusurika kwa kuwa

A.     Ilikuwa ukufundishwa kuhusu utabiri

B.     Haikufanya biashara na madereva

C.     Ilizingatia maadili na mashauri

D.    Mkazeni alikuwa mtabiri

  1. Kichwa kifaacho zaidi kueleza kifungu hiki ni:

A.     Mkazeni wa Tujueni na utabiri wake

B.     Asiyesikia la mkuu huvunjika guu

C.     UKUMWI utaangamiza watu wengi

D.    Mchelea mwana kulia hulia mwenyewe


Soma taarifa hii kisha ujibu maswali 41 mpaka 50

Maendeleo ya nchi hutegemea mchango na juhudi za kila mwananchi. Hata hivyo, ni jambo la kusikitisha kuona kuwa baadhi yetu tuna fikira zisizo za kizalendo kuwa wengine ndio wanaopasa kuiendeleza nchi. Watu wa aina hii hutarajia serikali kuwafanyia hili na lile. Huwathubutu kujiuliza je, mimi nimeifanyia nini nchi yangu?

Inafaa tukumbuke kwamba nchi ni kama chombo cha usafiri na kila mtu ana wajibu wa kuhakikisha kwamba chombo hicho kimekwenda ipasavyo. Tunahitaji kuwa na bidii za mchwa za kujenga kichuguu. Tuwe na umoja wa nyuki ambao, japo ni viumbe wadogo hudiriki kutengeneza asali ambayo huwafaa wao na kuwalisha binadamu. Ikiwa vidudu hivi vinaweza kuilisha jumuiya, sembuse sisi?

Mungu amemtunukia kila mmoja wetu vipawa anuwai. Ni juu yetu kuvitumia vipawa hivi kuinua uchumi wa nchi. Tukujitahidi pamoja tutaweza kutatua matatizo mengi yanayoikumba nchi. Tukumbuke kwamba kinga na kinga ndipo moto uwakapo. Wananchi katika nyanja mbalimbali hawana budi kuziimarisha nyanja hizi ili kuinua hali zao za maisha. Mathalani, wakulima watumie njia za kisasa za ukulima ili kuzalisha mazao mengi. Wakifanya hivyo, tutaweza kukabiliana na baa la njaa ambalo linawadhuru wananchi wengi.

Vijana nao wana jukumu lao kwa taifa. Wewe kama mwanafunzi, unaweza kuchangia maendeleo ya nchi hii kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli zote za shule. Ujibidiishe vilivyo, si katika masomo pekee, lakini pia katika michezo. Kwa kuiendeleza michezo ya riadha na hata ya kuigiza, utakuwa umeiendeleza nchi kwa kuukuza utamaduni wako. Isitoshe, unaweza kushiriki katika shughuli za kuzoa taka katika mtaa ulio karibu na shule yako. Ukifanya hivyo utakuwa umeitikia wito wa serikali wa kuhufadhi mazingira.

Sehemu za mashambani zinahitaji kushughulikiwa kimaendeleo. Licha ya kuwa sehemu nyingi zina rutuba, vijana wengi baada ya kupata masomo huhiari kuhamia mjini kutafuta kazi zenye hadhi. Mashamba yameachiwa wazee na bila shaka mazao yamekuwa haba. Hebu tujiulize, je, ikiwa sisi vijana tutaziacha sehemu zetu na kuhamia kwingine, nani atakayeziauni? Je, hatujui kuwa chetu ni chetu na nguo ya kuazima haifai chochote? Ni vyema tukumbuke kuwa ikiwa tunataka kusaidiwa kuendeleza sehemu zetu, ni lazima sisi wenyewe tuwe tayari kuzitumikia kwani abebwaye hujikaza. Mapenzi kwa nchi ni muhimu mno. Shime tuungane kuijenga nchi yetu.


  1. Maendeleo ya nchi yanahitaji

A.     Kushughulikia kila mara katika kilimo

B.     Ushirikiano wa kila mwananchi

C.     Kutotarajia serikali kufanya lolote

D.    Watu wengine kuendeleza nchi

  1. Watu walio na fikra za kizalendo ni wale

A.     Wanaotarajia kusaidiwa kila mara

B.     Wanaowataka wengine kushughulikia miradi ya maendeleo

C.     Wasiojua wameifanyia nini nchi

D.    Wasiopuuza wajibu wao katika kuendeleza nchi

  1. Nchi ni kama chombo ch usafiri kwa sabau:

A.     Wananchi wasipoendeleza nchi itazorota

B.     Bila chombo usafiri haufanikiwi

C.     Wananchi wasiporudi mashambani nchi itazorota

D.    Bila wasafiri nchi haifanikiwi

 

  1. Binadamu wanalinganishwa na nyuki kwani

A.     Wakiwa na bidii nyingi wanaweza kujifaidi wao na wengine

B.     Nyuki wana umoja japo ni viumbe wadogo

C.     Wakiwa na umoja na bidii wanaweza kujifaidi wao na wengine

D.    Nyuki na mchwa wana bidii za kujenga

  1. Katika kifungu, matendo yanayoonyesha ukweli wa methali, “Kinga na Kinga ndipo moto uwakapo” ni

A.     Vijana kuzoa taka na sote kushiriki katika michezo

B.     Wote kurudi mashambani na kulima kwa bidii

C.     Vijana kudumisha utamaduni na kuimarisha elimu

D.    Ushirikiano wa nyuki na wananchi kujitahidi pamoja

  1. Kulingana na kifungu, matatizo mengi yatatatuliwa iwapo

A.     Tutafanya kazi kwa pamoja bila kuzingatia tofauti zetu

B.     Sote tutakuwa na vipawa tofauti tofauti

C.     Sote tutajibidiisha katika masomo yetu

D.    Tutatarajia misaada kuinua hali za maisha yetu

  1. Vijana

A.     Wanapaswa tu kushughulikia masomo

B.     Wanapaswa kusoma ili kukuza utamaduni

C.     Wanapaswa kushiriki kuiimarisha nchi katika nyanja mbalimbali

D.    Wanapaswa kushirikiana wao kwa wao kujiinua na kuimarisha kilimo

  1. Kulingana na kifungu maana ya kazi zenye hadhi ni

A.     Kazi zinazolipa mishahara mikubwa

B.     Kazi zinazofikiriwa kuwa bora kuliko za mashambani

C.     Kazi zenye marupurupu mengi kuliko za mashambani

D.    Kazi za walio na elimu ya juu

  1. Kulingana na kifungu hiki, abebwaye hujikaza ina maana

A.     Unaposaidiwa lazima nawe pia ujitahidi

B.     Ukibebwa mgongoni usilegee kamwe

C.     Tusitarajie kusaidiwa bila kusaidia

D.    Tukiwasaidia wengine lazima tujitahidi

  1. Ikiwa vidudu hivi vinaweza kulisha jumuiya, sembuse sisi? Maana yake ni
  1. Nyuki wanaweza kulisha watu wengi
  2. Binadamu ana uwezo wa kushirikiana
  3. Nyuki wana ushirikiano kuliko binadamu
  4. Binadamu wana nguvu za kuzalisha kuliko nyuki

 


2006 ANSWERS 1 

icon envelope tick round orange animated no repeat v1 Virus-free.www.avast.com

Print Friendly, PDF & Email
people found this article helpful. What about you?

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x