KCPE PAST PAPERS 2009 KISWAHILI QUESTIONS AND ANSWERS

MARKING SCHEME 2

KCPE PAST PAPERS 2009 KISWAHILI QUESTIONS AND ANSWERS

 Manyam Franchised Tests

KISWAHILI   |   KCPE   |   2008

 

NAME…………..……………..…………. SCHOOL…………….…………………DATE……………… TIME: 2 hours


Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa

            Kwa __1__ Kiswahili ni lugha ya Kiafrika ambayo imeenea kote. Wenyeji asilia__2__wakiongea lugha hii__3__awali ni Waswahili. Waswahili wanapatikana kote katika upwa mzima__4__pwani ya Afrika Mashariki. Kwa muda mrefu Kiswahili__5__humu nchini lakini mambo yamebadilika. Lugha hii sasa imepewa hadhi kubwa __6__nyanja mbalimbali nchini. Lugha hii__7__pakubwa kuwaunganisha wananchi na kudumisha amani. Wakenya wengi wamejitolea kuikuza lugha hii yao na hawataki tena__8__

            A                                 B                                  C                                  D

  1. Sababu                         hivyo                            hakika                          vile
  2. Wamekuwa                   waliokuwa                    watakaokuwa                wangekuwa
  3. Tangu                           hadi                              hata                              mpaka
  4. Wa                               kwa                              ya                                 mwa
  5. Hakikudhaminiwa         haikuthaminiwa             hakikudhaminiwa          hakikuthaminiwa
  6. Katika                          kati ya                          ndani ya                        kuliko
  7. Imechanga                    imechangiwa                 imechangia                   imechangisha
  8. Kuizungumza                kuitwaza                       kuitumia                       kuididimiza

Arusi ya Hadija__9__kijijini mote. Nyimbo zilisikika kwa siku tatu mfululizo. Vigoli na maghulamu walicheza ngoma bila kusita__10__ya magari ilionekana__11__kuelekea msikitini kwa sherehe ya kufunga ndoa. Kijiji chote kilijaa wageni__12__kutayarisha arusi. Nyumba ya bibiarusi ilijaa mapambo tele na kuta__13__kupakwa rangi ya kupendeza. Arusi ikawa ya kufana mno. Watu__14__. Hata baada ya__15__nilienda nikijisemea kimoyomoyo, “Jambo la heri huenda kwa heri. Mola awajalie mema.”

A                                 B                                  C                                  D

  1. Ilitia chumvi                 ilitia for a                      ilipiga mbiu                  ilipiga debe
  2. Safu                             milolongo                     msongamano                 mistari
  3. Ikiandamana                 ikifuatia                        ikifuatwa                      ikiandama
  4. Walivyokuja                 walipokuja                    waliyokuja                    waliokuja
  5. Yoyote                         yote                              zote                              zozote
  6. Wameiajabia                 wanaiajabia                   wakaiajabia                   wakiiajabia
  7. Kutangamana                kujumuika                     kufungamana                kufumukana


 

 

Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu lililo sahihi

  1. Chagua usemi wa taarifa ulio sahihi

“Kilele cha Mlima Kenya kina theluji nyingi,” Fatuma akasema.

A.    Fatuma alisema kwamba kilele cha mlima Kenya kilikuwa na theluji nyingi

B.     Fatuma anasema kwamba kilele cha mlima Kenya huwa na theluji nyingi

C.     Fatuma akasema kwamba kilele cha Mlima Kenya kimekuwa na theluji nyingi

D.    Fatuma alisema kwamba kilele cha Mlima Kenya kingekuwa na theluji nyingi

  1. Ni sentensi ipi inayoonyesha matumizi sahihi ya lau?

A.    Lau mwanafunzi anapopita mtihani hutuzwa

B.     Lau ungekuja ningekusaidia

C.     Nipe lau kitabu kimoja nisome

D.    Nitakujuza lau hutaki kujua

  1. Chagua jibu linaloonyesha aina za mashairi

A.    Tarbia, takhmisa

B.     Tarbia, mizani

C.     Vina, takhmisa

D.    Takhmisa, mishororo

  1. Chagua kinyume cha sentensi

Musa alisifiwa kwa utiifu wake

A.    Musa hakusifiwa kwa utiifu wake

B.     Musa alikashifiwa kwa utundu wake

C.     Musa alikashifiwa kwa ukaidi wake

D.    Musa hakukashifiwa kwa ukaidi wake

  1. Methali yenye maana sawa na “usiache mbachao kwa msala upitao” ni

A.    Usione kwenda mbele kurudi nyuma si kazi

B.     Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi

C.     Usipoziba ufa utajenga ukuta

D.    Bura yangu sibadili na rehani

  1. Jogoo ni kwa koo, fahali ni kwa

A.    Ndama

B.     Kipora

C.     Tembe

D.    Mtamba

  1. Chagua aina ya pambo ambalo huvaliwa miguuni

A.    Kipete

B.     Kidani

C.     Kikuku

D.    Kikuba

  1. Umoja wa sentensi, “Wangwana wowote hawawezi kutufanyia fujo” ni

A.    Muungwana yeyote hawezi kutufanyia fujo

B.     Muungwana yeyote hawezi kunifanyia fujo

C.     Muungwana yoyote hawezi kunifanyia fujo

D.    Muungwana yoyote hawezi kutufanyia fujo

  1. Chagua sentensi ambayo ni muungano sahihi wa hizi

Mburukenge aliingia uwanjani

Mburukenge aliwafadhaisha wanafunzi

A.    Mburukenge aliingia uwanjani na kuwafadhaisha wanafunzi

B.     Mburukenge aliingia uwanjani kwa kuwafadhaisha wanafunzi

C.     Mburukenge aliingia uwanjani lakini aliwafadhaisha wanafunzi

D.    Mburukenge aliingia uwanjani kwani aliwafadhaisha wanafunzi

  1. Kumpiga mtu vijembe ni

A.    Kumpa sifa asizostahili

B.     Kumsema kwa mafumbo

C.     Kumchafulia mtu jina

D.    Kumfanyia ishara ya dharau

  1. Ugonjwa wa ukambi pia huitwa

A.    Surua

B.     Safura

C.     Ndui

D.    Tetewanga

  1. Sahihisha: kule mlikolima hamna rutuba

A.    Kule mlipoima hamna rutuba

B.     Pale mlipolima hamna rutuba

C.     Kule mlikolima hakuna rutuba

D.    Mle mlimolima hakuna rutuba

  1. Chagua nomino kutokana na kitenzi kumbuka

A.    Kumbukika

B.     Kumbukwa

C.     Kumbusha

D.    Kumbusho

  1. Umbu, mkoi, halati, wote ni

A.    Jamii

B.     Wakwe

C.     Jamaa

D.    Marafiki

  1. Kitendawili. “Nikitembea yuko, nikikimbia yuko nikiingia ndani hayuko,” jibu lake ni

A.    Mwanga

B.     Kivuli

C.     Mwangwi

D.    Upepo


Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31-40

      Uamuzi uliofanywa na serikali wa kuhimiza watoto wote warudi shuleni ni jambo mwafaka. Watoto walifurika furifuri shuleni ili kusajiliwa. Wale waliokuwa wakirandaranda mitaani walifuatiliza himahima na kupelekwa shule. Waliokuwa wakubwa ki-umri walipelekwa shule za ufundi. Wakatabasamu kwa furaha kama mzazi aliyepata salama.

      Kwa miaka mingi, baadhi ya wazazi walikuwa wzmeshindwa kuwasomesha wana wao. Hii ni kutokana na umaskini uliokithiri mipaka. Hali hiyo ilichangia huzuni kuu miongoni mwa familia. Pengo la waliosoma na wasiosoma lilizidi kuwa pana kielimu na kiuchumi. Uadui ukaingilia jamii. Ujambazi nao ukazidi.

      Sasa watu wote wakipewa haki sawa ya kusoma, hata wale watoto wa maskini watamanio masomo watakinaisha kiu yao. Pia mengi ya matatizo yatapungua. Si kweli kuwa tajiri ni mwerevu kuliko mkata. Kila mwanajamii akipewa nafasi na asome kwa bidii atafua dafu maishani.

      Vijana watakaofuzu katika shule za kiufundi wataweza kuajiriwa katika sekta mbalimbali. Mwishowe wakipata mtaji watajiendeleza kwa kuanzisha miradi midogomidogo ya kujitegemea. Hali kama hii ikienea kote nchini viwanda vidogvidogo vitaanzishwa na ajira itapatikana. Hiyo itakuwa njia mojawapo kuu ya kuuinua uchumi wa kuzalisha nafasi nyingi za kazi. Kitaaluma, hawa vijana wataweza kuwa madaktari, wasanii, walimu… na kazi zingine nyingi. Kisomo ni kitamu. Hakifai kutiliwa nanga.

 


  1. Uamuzi uliofanywa na serikali

A.    Ulisababisha kufurika kwa watoto shuleni na kupita mitihani

B.     Ulisababisha kuchipuka kwa vyuo vya ufundi na kuondoa umaskini

C.     Ulisababisha kuongezeka kwa watoto shuleni na kupata nafasi ya kujiendeleza

D.    Ulisababisha kupungua kwa umaskini na kuwapa watoto nafasi ya kujiendeleza

  1. …baadhi ya wazazi walikuwa wameshindwa kuwasomesha wana wao

Chagua methali inayoweza kueleza hali hii

A.    Maskini kupata ni mwenye nguvu kupenda

B.     Dua la mnyonge haliendi joshi

C.     Ngombe wa maskini hazai pacha

D.    Maskini halali mchana

  1. Ukosefu wa elimu unasababisha

A.    Umaskini, uadui, huzuni na ujambazi

B.     Wivu, ujambazi, kukosa kiu ya kusoma na uadui

C.     Utajiri, ukosefu wa kazi, huzuni na ujambazi

D.    Ujambazi, wivu, utajiri na kiu ya kusoma

  1. Kulingana na kifungu, pengo kubwa la kiuchumi limesababishwa na

A.    Watoto kutopata kisomo kwa sababu ya umaskini

B.     Uadui na ujambazi ulioikumba jamii maskini

C.     Watoto kutopelekwa shule za ufundi kwa sababu ya umaskini

D.    Wazazi kushindwa kupambana na umaskini

  1. Ni kweli kuwa watu wote wakipewa nafasi sawa

A.    Watoto wa maskini watakuwa werevu

B.     Watoto maskini na tajiri watakuwa sawa

C.     Watoto wote wapendao kusoma watakuwa matajiri

D.    Watoto wote wapendao kusoma watapata kisomo

  1. Vijana wote wakipata mtaji

A.    Wataanzisha miradi ya kiufundi

B.     Wataweza hata kuwa wataalamu

C.     Wataanzisha shughuli za kujikimu

D.    Watakitilia kisomo chao makini

  1. Kisomo hakifai kutiliwa nanga kwa sababu

A.    Watu watakuwa wataalamu

B.     Kina manufaa mengi

C.     Shule zitapanuka

D.    Serikali itakigharamia

  1. Maana ya kusajiliwa ni

A.    Kurekebishwa

B.     Kunufaishwa

C.     Kuandikishwa

D.    Kufundishwa

  1. Watakinaisha kiu yao ina maana ya

A.    Watapunguza tamaa yao

B.     Wataacha hofu yao

C.     Watafurahia hali yao

D.    Watatosheleza hamu yao

  1. Kichwa kinachofaa zaidi kwa taarifa hii ni

A.    Ukarimu wa serikali

B.     Kupunguza ujinga

C.     Masomo ya kiufundi

D.    Serikali kupanua masomo


Soma taarifa hii kisha ujibu maswali 41 mpaka 50

      Wanafunzi wa shule ya Mtepetevu walitembelewa na wazazi. Kabla ya kuruhusiwa kukutana na watoto wao, wazazi waliingia kwenye mkutano. Takriban kila mzazi alimbebea mwanawe furushi la chakula, licha ya kuwa watoto wao walikuwa wamerudi kutoka nyumbani majuma mawili tu yaliyopita.

      Mkutanoni wazazi walizozana kuhusu maakuli shuleni, mavazi na mitindo ya nywele ya watoto hao. Baadhi walitaka watoto wao wapewe mapochopocho na matunda ghalighali. Wengine wao siku hiyo hawakufikiria sana kuhusu juhudi za watoto masomoni, kinyume na kawaida yao. Hata hivyo, wengi wao waliona mbele, wakapinga udekezaji huo.

      Mzozo ulipokuwa ukipamba moto, kijana mmoja wa karibu  miaka ishirini na minne, aliyekuwa amevalia kilalahoi, akaingia mkutanoni. Baadhi ya wazazi waliomuona walishindwa kwani mkutano ulikuwa wa wazazi. Kijana akaketi na kutega sikio. Mzazi mmoja alisimama na kusema, “Nimeitazama orodha ya vyakula na nimekasirika. Kwa nini hawa watoto hawapewi chapati kwa kima, pilau na ‘matoke’? Tunalipa! Sasa kwa nini wanakula ugali na ‘githeri’?”

      Kijana yule alikereketwa, akanyoosha mkono juu sana  na alipoona anapuzwa, akasimama na kuanza kusema, “Hoja mnazotoa si…” Baadhi ya wazazi wakamdakia na kusema, “We! Nyamaza. U mtoto! Mkwe wetu…” kijana akazidi kukawana na kutaka kupewa nafasi lakini wale waliokuwa karibu naye wakamlazimisha kuketi. Mwenyekiti akasema, “Huu ni mkutano wa wazazi. Jukumu lako kijana ni kunyamaza na kusikiliza kwa makini, kisha uwapelekee wazazi ujumbe.”

      Kijana alikazana, “Tafadhali nipeni ruhusa. Kitanda msichokilalia hamuwajui kunguni wake.” Akaulizwa walikokuwa wazazi wake kwani ndio waliotakiwa mkutanoni. Akajibu, “Bwana Mwenyekiti, sina wazazi! Mimi ni mlezi wa wadogo zangu, nina mdogo wangu hapa. Nimtoka mbali huko kote kuja kuawawakilisha marehemu wazazi wangu. Mimi si mlevi, si mhuni au mkwe wenu. Nina akili razini. Kuwa kijana si dhambi. Nimemaliza chuo kikuu. Nina kazi lakini mshahara wote unaishia kwenye malezi na sasa mnanikataza kusema lolote. Je, kijana hana haki? Ninajua kuwa maji hayazuiliki lakini tushirikianeni kwani penye wengi hapaharibiki neno.”

      Mwenyekiti akampa nafasi ya kujieleza. Kijana akaendelea, “Mimi kama kijana mlezi, nimewasikiliza kwa makini. Ninapinga hoja ya mavazi ya nyumbani na mapochopocho kama chapati… jambo linalofaa ni kuwafunza kutafuta elimu kwa bidii. Wakihimizwa kuwa na adabu na kuwa na kiu ya masomo, watajikataza wenyewe kufuata tu raha maishani. Kula bila kujua kutafuta Kutawatia mashimoni. Mvumilivu hula mbivu. Kugeuza mandhari ya shule kuwa ni sehemu ya mandhari kutajenga uvivu, wizi, matabaka na wivu shuleni. Wanafunzi watawabeza walimu, badala ya kuwasikiliza. Tuwafunze kujitegemea.” Wazazi walimhurumia na kumpigia makofi. Mwenyekiti akamuomba msamaha na kumshukuru kwa niaba ya wazazi.


  1. Ni jambo gani linaloonyesha kuwa hawa watoto wanadekezwa?

A.    Ingawa walikuwa hawajakaa sana shuleni, wazazi waliwabebea mafurushi ya vyakula

B.     Walikuwa wametoka nyumbani na mafurushi ya vyakula

C.     Wazazi walikuwa wanataka watoto wale mapochopocho, sio tu kuvaa kifahari

D.    Wazazi walikuja mpaka shuleni kuwaona watoto hao na vyakula

  1. Ukipamba moto maana yake ni

A.    Ukiwa na joto jingi

B.     Ukizidi kuendelea

C.     Ukuharibika

D.    Ukuhimizwa

  1. Mkutanoni kulikuwa na

A.    Wapinzani, mwenyekiti na kijana

B.     Waungaji mkono, kijana na mwenyekiti

C.     Wageni, kijana na mwenyekiti

D.    Wadekezaji, waona mbele na mwenyekiti

  1. Kijana alipuuzwa kwa sababu ya

A.    Mavazi yake

B.     Mazungumzo yake

C.     Umri wake

D.    Kutaka kuongea

  1. Kwa nini kijana alikazana kunyoosha mkono?

A.    Alitaka kuondoa shaka ya wazazi na kutoa hoja zake

B.     Alitaka kusema kuwa yeye ni mlezi si mkwe

C.     Alikasirika na kutaka kupingana na wazazi

D.    Alikasirika kwa kudharauliwa akataka ajitambulishe 

  1. Hoja za kijana zilionyesha

A.    Ukaidi wake

B.     Ulala hoi wake

C.     Ukomavu wake

D.    Ujana wake

  1. Kulingana na kifungu kitanda msichokilalia hamuwajui kunguni wake ina maana

A.    Wazazi hawajajua matatizo ya watoto

B.     Wazazi hawakujua hali ya kijana

C.     Wazazi hawakuamini hoja za kijana

D.    Wazazi hawakuamini maoni ya watoto

  1. Kulingana na taarifa hii wazazi walipaswa

A.    Kujadili jinsi watoto wao walivyokula, walivyovaa na kuwa na mandhari shuleni

B.     Kuzungumzia nidhamu ya jinsi ya kuwahimiza walimu kuwapa watoto chakula cha kifahari

C.     Wakomeshe udekezaji, wahimize nidhamu na kuacha kutaka kugeuza shule kuwa ni mandari

D.    Kuondoa udekezaji na raha zote zilizokuwapo shuleni kama mavazi ya kifahari na lishe bora

  1. Mpangilio bora wa matukio ya siku hiyo huko Mtepetevu ulikuwa

A.    Kuwasili, kuingia mkutanoni, kuzozana, kuelewana na kuomba msamaha

B.     Kuwasili, kuzozana, kuomba msamaha, kuingia mkutanoni na kuelewana

C.     Kuwasili, kuingia mkutanoni, kuelewana, kuzozana na kuomba msamaha

D.    Kuwasili, kuzozana, kuingia mkutanoni, kuomba msamaha na kuelewana

  1. Kichwa mwafaka kinachofaa kueleza taarifa hii ni

A.    Dhifa ya wazazi shuleni

B.     Ujana shuleni si hoja

C.     Mzozo na mapatano shuleni

D.    Kudunishwa kwa vijana shuleni

 

MARKING SCHEME 2

icon envelope tick round orange animated no repeat v1 Virus-free.www.avast.com

Print Friendly, PDF & Email
people found this article helpful. What about you?

Leave a Reply 0