KCPE PAST PAPERS 2007 KISWAHILI LUGHA QUESTIONS AND ANSWERS

KCPE PAST PAPERS 2007 KISWAHILI LUGHA QUESTIONS AND ANSWERS

 Manyam Franchised Tests

KISWAHILI   |   KCPE   |   2007

 

NAME…………..……………..…………. SCHOOL…………….…………………DATE……………… TIME: 2 hours


Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa

            Kilimo ni sekta muhimu __1__. Baada ya mimea kuchipuka, mkulima hana budi __2__ ili kuikinga dhidi ya magugu na vimelea vingine ambavyo__3__ vikawa hatari kwa mimea. __4__ pia huendelezwa katika sehemu nyingine. Wanyama hawa huogeshwa ndani ya __5__ ili kuwauwa wadudu waharibifu. Kilimo kikiendelezwa sehemu za mashambani tutapunguza __6__ mjini wa watu wanaotafuta kazi. Vijana wanaokipuuza kilimo watiwe __7__kuzistawisha sehemu zao.

            A                                 B                                  C                                  D

  1. Kati ya nchi                  katika nchini                 katika nchi                    kati ya nchini
  2. Kuipogoa                      kuipalilia                      kuipura             kuipulizia
  3. Huja                             vimekuja                       vimeenda                      huenda
  4. Ufugaji                         ufungaji                        uwekaji             uwekezaji
  5. Vidimbwi                     majosho                        mito                             maziwa
  6. Uhamaji                        uhamishaji                    uhamishwaji                  uhamiaji
  7. Hima                            hamnazo                       shime                           kapuni

Msichana alikuwa amechoshwa na vitimbi vya kasri __8__ shangazi yake ambaye alikuwa amemtoa kijijini kuja kumpeleka shule. __9__ alikuwa na nia ya kumfanya __10__. Hakujua amlaumu shangazi yake huyu,__11__ majaliwa __12__ wazazi wake na kumwacha yatima. Alikumbuka jinsi __13__ na matumaini ya kusoma kwa bidii ili kuiokoa jamii __14__ kutokana na umaskini __15__ hali zao.

A                                 B                                  C                                  D

  1. La                                ya                                 mwa                             kwa
  2. Naam                           ndio                              maadamu                      kumbe
  3. Kitwana                        kijakazi             kuli                              kaimu
  4. Ila                                wala                             au                                 lau
  5. Aliyewachukua waliwachukua               yaliwachukua                yaliyowachukua
  6. Alivyokuwa                  aliyekuwa                     aliyokuwa                     alipokuwa
  7. Zake                             wake                            yake                             lake
  8. Uliyoizorotesha uliozizorotesha  ulioizorotesha                uliolizorotesha

           

 


Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu lililo sahihi

  1. Ni tasbishi ipi inayoafikiana na maelezo

“Kutokeza na kuendelea vizuri kwa haraka?”

A.    Chipuka kama majani

B.     Chanua kama waridi

C.     Chanua kama mgomba

D.    Chipuka kama uyoga

  1. Kitenzi nawa katika kauli ya kutendesha ni:

A.    Nawika

B.     Nawia

C.     Navya

D.    Nawisha

  1. Chagua wingi wa:

Baharia huyu hodari ni mgeni huku kwangu

A.    Baharia hawa hodari ni wageni huku kwetu

B.     Mabaharia hawa hodari ni wageni huku kwetu

C.     Mabaharia hawa hodari ni wageni huku kwangu

D.    Baharia hawa hodari ni wageni huku kwangu

  1. Chagua maneno ambayo yote ni vihisishi

A.    Ala, ee, wee, lo

B.     Vile, lo, simile, mashalla

C.     Jamani, huree, ingawa, isipokuwa

D.    Vyema, ila, inshalla, aa

  1. Chagua sentensi iliyo na kivumishi cha sifa

A.    Mwanafunzi ameandika insha nyingine

B.     Daktari amewatibu wagonjwa watatu

C.     Mpishi amepika chakula kibichi

D.    Mtoto yule anaweza kukimbia

  1. Chagua jibu ambalo ni nomino ya dhahania

A.    Wayo

B.     Umati

C.     Mate

D.    Wema

  1. Salamu “Alamsiki” hujibiwaje?

A.    Bi nuru

B.     Shabalkheri

C.     Salama

D.    Masalkheri

  1. Chagua usemi halisi wa:

Mwalimu aliwauliza kama wangeandika insha siku hiyo jioni

A.    “Mtaandika insha kesho jioni?” Mwalimu aliwauliza

B.     “Kesho jioni mngeandika insha?” Mwalimu aliwauliza

C.     “Mtaandika insha leo jioni?” Mwalimu aliwauliza

D.    “Leo jioni mngeandika insha?” Mwalimu aliwauliza

  1. Jina wanaloitana ndugu wa kike na wa kiume ni

A.    Somo

B.     Umbu

C.     Mnuna

D.    Kaka

 

  1. Chagua vielezi katika sentensi

Alisimama wima na kumwita kwa sauti

A.    Alisimama, kumwita

B.     Na, kumwita

C.     Wima, kwa sauti

D.    Kumwita, sauti

  1. Tegua kitendawili

Baba akipiga mbizi huibuka na ndevu nyeupe

A.    Muwa

B.     Kinu

C.     Mbegu

D.    Mwiko

  1. Pesa za ziada anazolipwa mkopeshaji ni

A.    Riba

B.     Ada

C.     Mshahara

D.    Ridhaa

  1. Maana ya methali

“Ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno” ni

A.    Jambo ambalo unaliona rahisi kwako kwa mwenzako huenda likawa gumu

B.     Haifai kudharau kitu chako duni kwa kutamani cha mwenzako

C.     Haifai kuwadharau watu waliokusaidia hapo awali, huenda ukawahitaji

D.    Kitu unachokiona duni kwako, huenda kikawa na manfaa kwa mtu mwingine

  1. Jaza pengo kwa kiunganishi kifaacho

Nitakusaidia___utahitaji msaada wangu

A.    Lakini

B.     Ingawa

C.     Iwapo

D.    Japo

  1. Mtu anayeihama nchi yake na kununua ardhi na kuishi nchi nyingine ni

A.    Mkimbizi

B.     Mlowezi

C.     Mtoro

D.    Msaliti


            Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 mpaka 40

            Nilizaliwa na kulelewa katika familia iliyotajika. Baba yangu mlajasho alikuwa tajiri wa mali ya moyo. Mimi na ndugu yangu mdogo hatukujua maana ya uhitaji kwani baba alitukidhia mahitaji yetu yote. Nyumbani mwetu kila siku mlisahiba na kutapika watu wa kila sampuli waliokuja kulilia hali kwa baba. Baba aliwasabilia kwa mengi. Kuna waliopewa ruzuku mbalimbali za vyakula, kuna waliopewa vibarua mashamba na waliofanya kazi pale nyumbani. Almuradi kila mwana kijiji alifaidika kutokana na mkono wazi wa baba. Ndugu yangu mdogo hakuisha kuwabughudhi waja hawa na kuwaita waegemea nundu.

Siku zilisonga na kupita kama maji ya mto; hata nikajipata katika katika shule ya msingi. Niliyakumbatia masomo yangu kwa hamu kubwa. Sikuwa na wakati wa kufanya ajizi, kwani baba, pamoja na pato lake nono, hakuwahi kudekeza hisia za ugoigoi. Nasi ilibidi tufuate nyayo zake; kwani mwana akibebwa hutazama kisogo cha nina. Nilifanya mtihani wangu wa darasa la nane na kuvuna nilichopanda. Asubuhi baada ya kutanazwa kwa matokeo ya mtihani huo,niliamshwa na sauti ya “pongezi mwanangu,” kutoka kwa baba. Baba alikuwa amebeba gazeti la siku hiyo, usoni amevaa tabasamu kubwa. Sikuamini maneno yake. Nilimnyang’anya gazeti na ikawa kweli mwenye macho haambiliwi tazama. Nilikuwa mwanafunzi bora nchini. Nilijiunga na shule mojawapo ya kitaifa.

Siku nilipokivuka kizingiti cha lango la shule ya kitaifa ya Tindi ndipo maisha yangu yalipoanza kuingia ufa, nilikutana na Tamasha, mwanafunzi machangamfu na mcheshi. Alijitambulisha kuwa alisomea shule iliyokuwa jirani na ile yangu ya msingi. Urafiki shakiki ukazaliwa kati yake nami. Tukawa daima tunaandamana. Hayo hayakunitia shaka, kwani tamasha alinihimiza kila mara nitie bidii masomoni. Hata hivyo, siku zilivyosonga ndivyo tabia yake ilivyonibainikia.

Jioni moja Tamasha alikuja chumbani mwangu akiwa amebeba unga aliouita dawa ya homa. Aliniambia nijaribu kutibu homa ambayo ilikuwa imenikaba kwa siku ayami. Nami, kwa kutotaka kumvunja rafiki yangu, nikachukua unga huo na kuutia kinywani; ingawa kwa kweli mwalimu wetu alikuwa ametuonya dhidi ya kutumia dawa zozote bila maelekezo ya daktari. Unga huu haukutibu homa yangu, ila ulinipa utulivu mkubwa wa akili, utulivu ambao sikuwa nimewahi kuushuhudia maishani.

            Tamasha alifika chumbani mwangu usiku kunijulia hali. Alinipata nimejituliza juu ya kitanda changu. Alinisalimu na kukenua kama aliyetarajia jawabu fulani kutoka kwangu. Nilimweleza hali yangu naye akaniambia kuwa ndivyo dawa hiyo ifanyavyo kazi; kwamba amekuwa akiitumia kwa muda, hata nyakati za mtihani; naye hupata nguvu za kukabiliana na majabali yote. Alinielekeza kwa mzee Kamaliza ambaye ndiye aliyekuwa akimuuzia unga huo. Kuanzia siku hiyo nikawa mteja mwaminifu wa Kamaliza. Nilitumia unga huu bila fikira nikidhani kuwa ilikuwa dawa ya homa tu! Sikujua ilikuwa dawa ya kulevya; na Tamasha alikuwa mraibu sugu wa dawa hiyo na nyingine nyingi! “uzuri wake huu ni wa mkakasi tu?” Nilijiuliza, “Laiti ningalijua,” Hata hivyo maswali yote haya hayakuwa na faida tena. Nilikuwa tayari nimezama katika tatizo sugu la matumizi ya dawa za kulevya.

Nilijisuta moyoni kwa matumizi ya dawa za kulevya ambayo yalielekea kuyagongesha mwamba maisha yangu shuleni. Hata hivyo, haikuwa rahisi kuacha kwani nilichelea kuitwa limbukeni na wenzangu. Matokeo ya haya yote yakawa kuzorota kwa masomo yangu. Walimu hawakuchelewa kuona mabadiliko yaliyonikumba. Walijaribu kunishauri na kutaka kujua kilichokuwa kikinisumbua. Walipoona kwamba hali yangu haibadiliki na kwamba nimeshindwa kuwaambia tatizo langu, walimjulisha mwalimu mkuu ambaye hakukawia kumwita baba.

Mazungumzo kati ya baba na mwalimu mkuu yalinitia fadhaa kubwa kwani sikutaka kumwaambia nilitumia dawa za kulevya; ingawa kwa kweli mwalimu mkuu alishuku. Walijaribu kunishika sikio kuhusiana na tabia hii yangu; lakini tangu lini sikio la kufa halisikii dawa? Niliendelea na uraibu wangu hadi siku nilipofunzwa na ulimwengu baada ya kufumaniwa na naibu wa mkuu wa shule nikipiga maji. Nilipewa adhabu niliyotarajia. Nilijipata nyumbani kwa muda wa mwezi mzima, nikiuguza vidonda vya moyo na akili. Kijiji kizima kilijua nimefukuzwa shule kwa sababu ya matumizi ya dawa za kulevya. Sikuwa na pa kuutia uso wangu. Hata hivyo hili lilikuwa funzo kubwa kwangu.

Mama yangu aliweza kunipa nasaha na kunishauri niache kutumia dawa hizo. Mara hii, maneno aliyoniambia yalikuwa na maana. Niliyasikiliza kwa makini. Hata baba alipopata barua kumwarifu aniregeshe shule, nilikuwa tayari kurudi na kuyaanza maisha upya. Nilikuwa nimeamua kujiunga na chama cha vijana wanaopigana na matumizi ya dawa shuleni.


  1. Mambo yanayoonyesha kuwa Mlajasho alikuwa tajiri wa mali na moyo ni:

A.    Kukidhi mahitaji ya wana, watu kumlilia hali

B.     Kukidhi mahitaji ya wana, kuwapa watu riziki

C.     Kukudhi mahitaji ya wana, kumkanya mwanawe

D.    Kukidhi mahitaji ya wana, watu kumfuata kwake

  1. “Ndugu yangu mdogo hakuisha kuwabughudhi waja hawa na kuwaita waegemea nundu,” inaonyesha kuwa ndugu mdogo alikuwa
  1. Mwenye uzushi
  2. Mwenye kujisifu
  3. Mwenye mapuuza
  4. Mwenye uchoyo
  1. Msimulizi alisoma kwa hamu kwa kuwa

A.    Alipenda masomo yake

B.     Baba yake alikuwa mkali

C.     Baba yake alikuwa mwenye bidii

D.    Alitaka kufuata nyayo za ndugu yake

  1. Kifungu “ndipo maisha yangu yalipoanza kuingia ufa” kinamaanisha:

A.    Maisha ya msimulizi yalianza kupata matatizo

B.     Maisha ya msimulizi yaliporomoka

C.     Maisha ya msimulizi yalianza kubadilika

D.    Maisha ya msimulizi yaliharibika

  1. Msimulizi hakutaka kuacha “unga” kwa sababu

A.    Alikuwa amezoea uraibu wa Kamaliza

B.     Hakutaka kumuudhi Tamasha

C.     Alichelea kuondolewa kundini na wenzake

D.    Alichelea kudunushwa na wenzake

  1. Mambo yanayoonyesha kuwa kifungu hiki kinapinga matumizi ya dawa za kulevya ni:

A.    Msimulizi kufukuzwa shule, msimulizi kujiunga na wanaopinga matumizi mbaya ya dawa shuleni

B.     Walimu kumshauri msimulizi, mama pamoja na mwalimu mkuu kumwonya msimulizi shuleni

C.     Kamaliza kuacha kuuza dawa, mama kumshauri msimulizi

D.    Walimu kugundua tatizo la msimulizi, msimulizi kuaibika shuleni

  1. Kulingana na kifungu hiki, jamii inakabiliana na tatizo la matumizi mabaya ya dawa kwa:

A.    Kuwapeleka watoto shuleni, matajiri kuwasaidia watu

B.     Ushirikiano kati ya wazazi na walimu, kuwajibika kwa vijana

C.     Ushirikiano kati ya wazazi na walimu, kuaibika kwa vijana

D.    Wazazi kwenda shuleni wanapoitwa, kuwajibika kwa vijana

  1. Methali ambayo haifai kujumlisha ujumbe wa taarifa hii ni:

A.    Nzai mbovu harabu ya nzima

B.     Mchezea tope humrukia

C.     Mtegemea nundu haachi kunona

D.    Mchovya asali hachovyi mara moja

  1. “Uzuri wake huu ni wa makasi tu?” ina maana Tamasha:

A.    Alikuwa mcheshi

B.     Alikuwa mnafiki

C.     Hakuweza kuaminika

D.    Hakuweza kutegemewa

  1. Msimulizi alikuwa “sikio la kufa” kwa sababu

A.    Hakupona homa baada ya kutumia unga

B.     Hakuacha uraibu wake baada ya kuonywa na baba na mwalimu

C.     Alifumaniwa na naibu wa mwalimu mkuu akipiga maji

D.    Alipata adhabu aliyotarajia baada ya kupiga maji


Soma taarifa hii kisha ujibu maswali 41 mpaka 50

      Mafunzo ya kuimarisha maadili katika jamii ni muhimu kinyume na hapo awali, sasa maadili ya jamii zetu yanazoroteka kwa kasi sana kiasi cha kushangaza. Mwingiliano mwingi kati ya mataifa ya Kiafrika na ya kigeniunaweza kuleta upungufu wa maadili. Watu wengi hufikiria kuwa upotovu wa maadili ndio ustaarabu ufaao. Kusifu na kuziiga nyendo mbaya huchangia upalilizi wa uozo wa tabia. Hali hii inaweza kuzifuja nchi hizi.

      Ni dhahiri shahiri kuwa umaskini wa nchi umewafanya vijana kwa wazee kutamani na kuzitafuta njia za mkato za kujitajirisha. Kwa kuingiwa na tamaa nyingi, wao huanzisha miradi ya kifisadi. Watu hao hufanya juu chini kutafuta mianya ya kujipenyezea fedha. Wao hufanya haya bila ya kujali madhara yanayoletwa na hizo pilkapilka zao. Hongo huzidi kuendelezwa ili kuficha hizo njama ambazo huwa hatari kwa usalama wa nchi na watu wake.

      Tamaa ikikithiri mpaka, bongo za fisadi hao hazitulii. Bali huenda kwa haraka isiyomithilika. Watu hujikweza wakitaka kuwafikia na kuwapita waliowatangulia kiuchumi. Mathalani, watu ambao hivi majuzi walionekana hoi ama watu wa kawaida, ghafla huonekana watu wa kuishi kitajiri huku wakijijengea majumba ya ghorofa katika mitaa ya kifahari. Kama hali hiyo ingeletwa na kushukiwa na nyota ya jaha, tungeelewa. Lakini kama utajiri huo unatokana na kufurisha mifuko kwa kuleta shoti ofisini, wakitumia wizi wa kalamu au kula mlungula, itabidi utiliwe shaka na kulaaniwa. Vijana ambao ndio wajenzi wa taifa wa leo na kesho wanapaswa kuvipuuza vitendo hivyo kwa sababu vinadhalilisha utu wa jamii.

      Serikali nyingi za Kiafrika hutafuta mikakati ya kukabiliana na ufisadi ili ziimarishe maadili. Mojawapo ya hiyo mikakati ni hatua ya serikali ya kuwahimiza wananchi kujaza fomu kuonyesha jumla ya rasilimali zao. Hata hivyo, wahusika katika ufisadi hutafuta vizingiti vya kuzizuia juhudi hizo za serikali.

      Ni bayana kuwa mtu hawezi kushindana na mkono mrefu wa serikali. Juhudi za kukomesha vituko vya ufisadi zimeanza kuzaa matunda. Tayari vielezo vya kupambana na ufisadi vimeanza kujidhihirisha vyenyewe. Hivi majuzi, vituko vya kujenga nyumba hafifu hapa nchini vilifuatiliwa unyounyo na wahusika kufunguliwa mashtaka; hasa baada ya watu kupoteza maisha yao na wengine kulemazwa walipoangukiwa na nyumba hizo. Kwa mfano, watu waliodai kuwa watajenga ghorofa tatu, walibadili nia na kujenga ghorofa zaidi. Walifanya hivyo baada ya kupata vibali vya pembe za chaki. Isitoshe, kwa kila kutaka kutajirika haraka walinunua na kuvitumua vifaa duni kinyume na kanuni za uhandisi. Mambo kama haya hujitokeza katika nchi nyingi barani Afrika. Nchi hizi sasa zimeamka na kukaza kamba katika kuupinga ufisadi huu.

      Ikumbukwe kuwa ufisadi unaotokana na ukosefu wa maadili ni hatari kubwa kwa nchi yoyote ile. Mienendo kama hii hufuja nchi husika. Ni vyema kuepuka tabia hizi kama mtu aepukavyo ugonjwa wa kuambukiza.


  1. Nchi zetu zinazidi kuharibiwa na:

A.    Kufuata ustaraabu wa kigeni na kupuuza maadili

B.     Wananchi wapendao maadili ya mataifa yao

C.     Vijana wanaoigiza maadili yafaayo

D.    Kutoelewa vizuri maana ya maadili

  1. Chagua maelezo yaliyo sawa kulingana na aya ya pili

A.    Njama za ufisadi zinailetea nchi matatizo

B.     Usalama wa nchi hautegemei pilkapilka za fisadi

C.     Maskini wote wanatafuta njama za kujitajirisha kifisadi

D.    Njia za mkato zatajirisha nchi upesi

  1. Ushahidi kuwa ufisadi upo ni

A.    Kuwapo na kuziiga nyendo za kigeni

B.     Kupatikana kwa haraka kwa mambo ya kifahari

C.     Kujenga majumba makubwa na ya kifahari katika mitaa bora

D.    Kupnekana kwa mabadiliko ya ghafla kiuchumi kwa waliotajika

  1. Utajiri unaotiliwa shaka ni ule

A.    Wa kuigwa na watu wote

B.     Usio na wizi wa kalamu

C.     Wa njama za uharibifu

D.    Upendwao na vijana nchini

  1. Kushukiwa na nyota ya jaha ni sawa na

A.    Mchezo wa bahati nasibu

B.     Kupewa zawadi kwa kushinda

C.     Kupata kwa haraka

D.    Kubahatika kihalali

  1. Kulingana na taarifa hii, mawazo ya fisadi

A.    Yanaimarisha nci kiuchumi kwa kutajirika

B.     Hayazingatii utamaduni wa wote

C.     Hutafuta njia mbalimbali za kujitajirisha

D.    Yanatamani maadili ya watangulizi wao

  1. Upalilizi wa uozo wa tabia huendelezwa kwa

A.    Kupenda na kuzifuata tabia za kifisadi

B.     Kufikiria tu juu ya upotovu wa maadili

C.     Kusifu na kuzifuata nyendo zote za kigeni

D.    Mwingiliano wa binadamu katika ustaraabu

  1. Madhara makuu yanayoweza kupata jamii ya kifungu ni

A.    Vijana kuupenda na kuuiga utamaduni wa kigeni

B.     Umaskini mkubwa unaorudisha nchi nyuma kiuchumi

C.     Watu kuingilia njama za kifisadi kwa kutaka kutajirika

D.    Maangamizi yanayotolewa na watu wenye njama za kifisadi

  1. Mwandishi wa taarifa hii ana msimamo kuwa

A.    Ustaarabu wote wa kigeni unapotosha maadili

B.     Maadili yatafaulishwa na vijana na serikali husika

C.     Uigaji wa nyendo za kigeni unapaswa kuzuiwa

D.    Ujenzi wa ghorofa duni na njama za kifisadi zimezidi

  1. Kifungu hiki kinaweza kufipishwa kwa kutumia methali

A.    Mwacha mila ni mtumwa

B.     Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe

C.     Tamaa mbele mauti nyuma

D.    Vyote ving’aavyo si dhahabu

 

icon envelope tick round orange animated no repeat v1 Virus-free.www.avast.com

Print Friendly, PDF & Email
people found this article helpful. What about you?

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x