WATU NA KAZI ZAO

 • MWANGALIZI
  mtu anayefanya kazi ya utunzaji na uhifadhi wa vitu ili visiharibike au mambo yasiende kombo
 • MWANGUZI
  mtu afanyaye kazi ya kuangusha matunda k.v-nazi kutoka mtini
 • MWANAFASIHI
  mtu anayefanya kazi ya uandishi wa sanaa ya fasihi
 • MWANAMKENDE/KISABALUU/KIBERENGE/KAHABA/MALAYA/KIBIRITINGOMA/CHANGUDOA/MTALALESHI/MLUPO/GUBERI
  mwanamke anayefanya kazi ya kujiuza au kuuza mwili wake kwa wanaume kwa ajili ya kupata pesa
 • MNDEWA/JUMBE
  mtu ambaye ni kiongozi wa jamii yake,pia huitwa balozi wa kijiji
 • MWANAMICHEZO
  mtu ambaye kazi yake ni michezo,mdau wa michezo
 • MWANAMASUMBWI/MWANANDONDI
  anayefanya kazi ya kupigana ndondi au ngumi
 • MWANAMUZIKI/MWIMBAJI
  mtu anayefanya kazi ya kuimba kwa kutumia zana za muziki
 • MWANARIADHA
  anayefanya kazi ya mbio;riadha.mchezaji wa riadha
 • MWANARIWAYA
  anayefanya kazi ya kuandika vitabu vya hadithi,novela au riwaya
 • MWANASARUFU
  mtu ambaye kazi yake hushughulikia taaluma ya sarufi
 • MWANASAYANSI
  mtu ambaye kazi yake inashughulikia uchunguzi,upimaji,majaribi
 • UTEDI
  mtumishi wa cheo kidogo afanyaye kazi katika chombo cha bahari k.v kukiosha na kuwapa watu chakula
 • MAMANTILIE
  mtu hasa wa kike anayeuza chakula magengeni au nyumbani
 • MAMLUKI
  huyu ni askari wa kukodiwa ili kupigana katika nchi jirani
 • HARAMIA
  huyu ni mnyang’anyi wa baharini.Gaidi wa baharini.
 • MAKANIKA
  fundi wa kutengeneza magari au mashine
 • MANAMBA
  wafanyakazi wahamiaji katika mashamba makubwa
 • MCHINJAJI
  mtu anayefanya kazi ya kuchinja wanyama na kuwauza kwenye bucha
 • MCHORAJI
  mtu anayefanya kazi ya kuchora picha
 • LUGOJO
  watu wanaolinda kwa zamu
 • MFAGIZI/MFAGIAJI
  mtu anayefagia
 • MFARISHI
  mtu anayefanya kazi ya kutandika kitanda
 • MRINA
  fundi stadi wa kupakua asali
 • RUGARUGA
  mtu ambaye anafanya kazi chini ya amri ya chifu
 • KIBICHAMBO
  mtu hasa wa kike anayetumiwa kufanya kazi ya kunasa adui wa upande hasimu
 • FUNDIBOMBA
  mtu atengenezaye mifereji ya maji
 • MKWEZI
  anayepanda au kuaramia miti kv minazi na kuangua nazi
 • MFUANAZI
  mtu anayetoa makumbi kwenye nazi
 • KOSTEBO
  polisi wa cheo cha chini…

 • MNAJIMU/FALAKI/MAJUSI
  mwenye elimu na stadi wa masuala ya nyota
 • MWANDAZI
  mtu anayepika chakula kwa ajili ya shughuli za fulani k.v-sherehe,karamu nk
 • MNYAPARA/MSIMAMIZI
  mtu anayeangalia au kusimamia utekelezaji wa kazi
 • MKADIMU
  msimamizi mkuu wa shamba
 • NOKOA
  msaidizi wa mkadimu
 • MHADHIRI
  mwalimu katika chuo kikuu au chuo cha kadri anayefundisha kwa kutoa mhadhara
 • MJUME
  fundi wa kutia nakshi katika vyombo kama vile vya madini au mbao
 • TARISHI/MJUMBE/KATIKIRO/MESENJA
  mtu anayefanya kazi ya kutumwa kupeleka barua au ujumbe kutoka ofisi moja hadi nyingine au mahali mbalimbali
 • MSHENGA
  mtu anayetumwa kupeleka ujumbe au habari za kuoa-posa kutoka upande wa mchumba-mume kwa upande wa mke-mchumbiwa
 • DAKTARI/TABIBU/MGANGA
  mtu stadi katika masuala ya kuwatibu wagonjwa
 • DAKTARIMENO/MHAZIGIMENO
  huyu ni daktari wa meno
 • KULI/MPAKUZI/MPAKIZI
  mtu anayefanya kazi ya kupakua na kupakia mizigo kwenye meli,gari,bohari au mahali panapostahili
 • MSUSI/MSONZI
  anayesuka watu nywele
 • KARII
  msomaji wa Kurani

 • MWALIMU/MDARISI/USTADH
  Mtu anayefundisha
 • NAHODHA
  mtu anayeendesha meli
 • SARAHANGI
  mtu anayemsaidia nahodha(nahodha wa pili)
 • KANDAWALA
  mtu anayeendesha garimoshi
 • DEREVA
  mtu anayeendesha gari
 • RUBANI
  mtu anayeendesha ndege
 • SAISI
  mtu anayefanya kazi ya kuchunga wanyama wanaopandwa kama vile Farasi,Punda,Ngamia n.k
 • MZEGAMZEGA
  mtu anayeuza maji kwa kuyatembeza
 • MGEMA
  mtu anayefanya kazi kukinga tembo la mnazi au kuchanja magome ili kupata utomvu au kutengeneza ulimbo
 • DALALI/MNADI
  mtu anayeuza bidhaa mnadani kwa kutangaza;**Zabuni-uza kwa kushindanisha bei
 • MACHINGA/MMACHINGA
  mtu anayefanya kazi ya biashara kwa kutembeza bidhaa zake aghalabu kwa miguu ili kuwatafuta wateja mf.’Malimali’
 • MCHUKUZI/HAMALI/MPAGAZI
  mtu anayefanya kazi ya kubeba mizigo kwa kutumia rukwama,toroli,bero/baro nk
 • MCHUUZI
  mtu afanyaye kazi ya biashara ya kuuza vitu rejareja mf.Hawker!
 • MKUNGA
  mtu anayewasaidia wanawake kukopoa au kujifungua
 • NGARIBA
  mtu anayetahiri vijana jandoni au unyagoni
 • MHASIBU
  Mtu anayefanya kazi ya upimaji wa hali ya kifedha ya shirika au biashara, Mtaalamu wa kuweka hesabu za fedha. ‘Accountant
 • MHAKIKIMALI
  anayefanya kazi ya kuhakiki ubora wa bidhaa
 • MWAMIAJI/MWAMIZI
  afanyaye kazi ya kuamia ndege shamba
 • MWAMUZI
  anayesuluhisha ugomvi baina ya pande mbili au zaidi
 • REFA/MWAMUZI
  anayechezesha mchezo kulingana na sheria za mchezo husika
 • MWANAANGA
  afanyaye kazi ya utafiti wa mambo ya anga
 • MWANABAYOLOJIA
  mtaalamu wa masuala ya viumbe na mimea
 • MWANADIPLOMASIA
  mtu anayefanya kazi kv katika ubalozi
 • MWANAGAINOKOLOJIA
  mtaalamu wa maradhi ya akina mama
 • MWANAISIMU
  mtaalamu wa masuala ya isimu na lugha
 • MWANAJESHI
  askari katika jeshi la ulinzi
 • MWANAMAJI/BAHARIA/MWANAPWA
  mtu anayefanya kazi katika chombo cha baharini
 • MWANASHERIA
  mtu utaalamu wa mambo ya sheria
 • MWANASIASA
  mtu anayejishughulisha na mambo ya siasa
 • MSHAIRI/MTUNZI/MALENGA
  mtu afanyaye kazi ya kutunga mashairi/nudhuma
 • MGHANI/MANJU
  gwiji katika kuimba mashairi
 • RAWI
  stadi katika kukariri au kusoma shairi bila kuimba
 • SHAHA
  mtu stadi katika kuhariri mashairi
 • MHARIRI
  stadi katika kusoma na kukosoa kazi ilioandikwa na mtu mwengine!
 • KARII
  mtu anayesoma Kurani hasa Tajuwidi
 • KONDAKTA/TANIBOI/UTINGO/MAKANGA
  mtu anayepokea nauli kwenye gari pia hupakia na kupakua mizigo kwenye matwana,daladala au matatu
 • MSUKAJI
  mtu anayeshona,kutarizi au kufuma mkeka,jamvi,kanda au vikapu
 • BOSI/TAJIRI
  mkuu wa ofisi anayeajiri watu katika kazi
 • MRAMALI
  mtu anayetabiri mambo kwa kuvmia elimu ya nyota
 • MRATIBU
  mtu anayepanga,kuunganisha na kusimamia shughuli za watu mbalimbali katika kazi au ofisi
 • HATIBU
  mtu anayetoa hotuba kwa hadhira au hadhara
 • BAYANA
  mtu stadi au fundi wa kusema,kuongea au kuhutubu kwa kutumia ujuzi wa lugha
 • MRASIMU
  mtu anayefanya kazi ya afisi na kulingana na taratibu na kanuni za utawala
 • WADENI
  mwenye dhamana ya kusimamia mahali k.v-mbuga za wanyama,hoteli,misitu,magereza
 • WAKALA/AJENTI
  mwakilishi wa kampuni,shirika au shughuli ya kibiashara
 • WARIA
  mtu aliye hodari katika kazi za mikono mf.ushonaji,uashi,uchongaji nk
 • UTEDI
  mtumishi wa cheo kidogo afanyaye kazi katika chombo cha bahari kv-kukiosha……………..

 • MWASHI
  mtu anayejenga nyumba za mawe;anayeaka
 • SAKUBIMBI
  mtu mwenye tabia za kueneza habari za watu za uongo
 • JASUSI/MPELELEZI/NDUNZI/DUZI/MTESI
  mtu anayechunguza watu kibubusa na matukio fulani katika nchi yake au nyingine
 • KIBARAKA/KIKARAGOSI
  kiongozi wa serikali anayetumiwa ili apate mamlaka au manufaa zaidi
 • MUALISAJI/MUUGUZI/NESI
  anayehudumia wagonjwa
 • BALOZI
  kiongozi wa kidiplomasia anayewakilisha nchi yake katika nchi nyingine
 • MLANGUZI
  mtu anayenunua bidhaa kwa bei rahisi na kuviuza kwa bei ghali
 • BEPARI
  mfanyabiashara mkubwa mwenye kumiliki rasilimali au mali na njia kuu za uchumi
 • MFINYANZI
  mtu anayeunda vyombo vya udongo k.v-vyungu,kauri nk
 • DIWANI
  mtu anayewakilisha watu wake katika serikali za mitaa
 • MKALIMANI/MTARIJUMANI/MTAPTA
  anayetafsiri lugha
 • SEREMALA
  fundi anayetengeza vifa vya mbao au fanicha au samani
 • MWADHINI
  mtu anayewaita watu msikitini kwa swala
 • TOPASI/CHURA
  mtu anayefanya kazi ya usafi wa choo
 • DOBI
  anayeosha nguo au kuzipiga pasi
 • SOGORA
  stadi wa kucheza ngoma…..

 • MHASIBU
  mtu anayeweka hesabu ya fedha
 • MHAZILI/SEKRETARI
  mtu anayetunza barua na majalada ya ofisi na kuandika kwa mashine kama vile taipureta au taipu
 • MHANDISI/INJINIA
  fundi wa mitambo hasa ya vyuma
 • BAWABU/GADI/MLINZI/ASKARIGONGO/SOJA
  mtu anayelinda mali na maisha ya tajiri au bwenyenye kv viwanda,boma,shule,mashirika,ofisi nk kwa kuweka usalama
 • MKUMBIZI
  mtu anayesafisha na kuondoa takataka;pia ni mtu afuataye wavunaji shambani na kuokoteza mavuno yaliyosalia na kuuza au kutumia nyumbani
 • MSAJILI
  mtu anayeandikisha vifo,kura na kuweka orodha ya kazi au vitu alivyokabidhiwa
 • SONARA/MFUAFEDHA
  fundi wa kutengeneza mapambo k.v-pete,kekee,mkufu,bangili,kikero n.k
 • MSANA/MHUNZI/MFUACHUMA
  mtu anayefanya kazi ya kufua vitu vya madini ya chuma au bati k.v-visu,sufuria,majembe,seredani,ndusi,panga nk
 • MUKUTUBI/MKUTUBU
  mtu anayefanya kazi ya kuhifadhi vitabu na kuviazimisha kwa wasomi
 • AKIDU
  mtu anayefanya kazi kwa mkatabani
 • MUTRIBU
  mtu anayeimba nyimbo za taarabu
 • MWASHI
  anayejenga nyumba….
 • MWANASAYANSI
  mtu ambaye kazi yake inashughulikia uchunguzi,ugunduzi,upimaji,majaribio na kuthibitishwa kwa muda uliopo
 • MWANASOKA
  mtu anayefanya kazi ya kucheza mpira wa miguu,soka,kabumbu,gozi au kandanda
 • MTAALAMU
  mtu anayefanya kazi taaluma aliyotaalamika ndani yake
 • MWANATAMTHILIA/MWANATAMTHILIYA
  mtu anayefanya kazi ya kuandika michezo ya kuigiza
 • MWANAHABARI/MTANGAZAJI
  mtu anayefanya kazi ya kutafuta,kuandika,kukusanya,kuhari na kutangaza au kusambaza taarifa au habari katika vyombo vya habari
 • MWANALEKSIKOLOGRAFIA
  mtu anayefanya kazi inayoshughulikia uchunguzi,uchambuzi na uchanganuzi wa msamiati wa lugha pamoja na maana yake
 • MLEHEMAJI
  mtu anayefanya kazi ya kuunganisha vitu hasa vyuma kwa kutumia madini aghalabu kwa kutumia risasi
 • MWANALEKSIKOGRAFIA
  mtu anayefanya kazi ya kuandika Kamusi
 • MSHAURINASAHA
  mtu anayefanya kazi ya kutoa ushauri au nasaha kwa watu
 • MCHANGANUZI
  mtu afanyaye kazi ya kuchanganua masuala tofautitofauti.
  Kwa hayo machache sina cha ziada.Je,una nini mdau?
 • MNAJIMU/FALAKI/MAJUSI
  mwenye elimu na stadi wa masuala ya nyota
 • MWANDAZI
  mtu anayepika chakula kwa ajili ya shughuli za fulani k.v-sherehe,karamu nk
 • MNYAPARA/MSIMAMIZI
  mtu anayeangalia au kusimamia utekelezaji wa kazi
 • MKADIMU
  msimamizi mkuu wa shamba
 • NOKOA
  msaidizi wa mkadimu
 • MHADHIRI
  mwalimu katika chuo kikuu au chuo cha kadri anayefundisha kwa kutoa mhadhara
 • MJUME
  fundi wa kutia nakshi katika vyombo kama vile vya madini au mbao
 • TARISHI/MJUMBE/KATIKIRO/MESENJA
  mtu anayefanya kazi ya kutumwa kupeleka barua au ujumbe kutoka ofisi moja hadi nyingine au mahali mbalimbali
 • MSHENGA
  mtu anayetumwa kupeleka ujumbe au habari za kuoa-posa kutoka upande wa mchumba-mume kwa upande wa mke-mchumbiwa
 • DAKTARI/TABIBU/MGANGA
  mtu stadi katika masuala ya kuwatibu wagonjwa
 • DAKTARIMENO/MHAZIGIMENO
  huyu ni daktari wa meno
 • KULI/MPAKUZI/MPAKIZI
  mtu anayefanya kazi ya kupakua na kupakia mizigo kwenye meli,gari,bohari au mahali panapostahili
 • MSUSI/MSONZI
  anayesuka watu nywele
 • MWASHI
  mtu anayejenga nyumba za mawe;anayeaka
 • SAKUBIMBI
  mtu mwenye tabia za kueneza habari za watu za uongo
 • JASUSI/MPELELEZI/NDUNZI/DUZI/MTESI
  mtu anayechunguza watu kibubusa na matukio fulani katika nchi yake au nyingine
 • KIBARAKA/KIKARAGOSI
  kiongozi wa serikali anayetumiwa ili apate mamlaka au manufaa zaidi
 • MUALISAJI/MUUGUZI/NESI
  anayehudumia wagonjwa
 • BALOZI
  kiongozi wa kidiplomasia anayewakilisha nchi yake katika nchi nyingine
 • MLANGUZI
  mtu anayenunua bidhaa kwa bei rahisi na kuviuza kwa bei ghali
 • BEPARI
  mfanyabiashara mkubwa mwenye kumiliki rasilimali au mali na njia kuu za uchumi
 • MFINYANZI
  mtu anayeunda vyombo vya udongo k.v-vyungu,kauri nk
 • DIWANI
  mtu anayewakilisha watu wake katika serikali za mitaa
 • MKALIMANI/MTARIJUMANI/MTAPTA
  anayetafsiri lugha
 • SEREMALA
  fundi au stadi anayetengeza vifa vya mbao au fanicha au samani
 • MWADHINI
  mtu anayewaita watu msikitini kwa swala
 • TOPASI/CHURA
  mtu anayefanya kazi ya usafi wa choo
 • DOBI
  anayeosha nguo au kuzipiga pasi
 • SOGORA
  stadi wa kucheza ngoma Kwa kutumia mkwiro.
 • MWANGALIZI
  mtu anayefanya kazi ya utunzaji na uhifadhi wa vitu ili visiharibike au mambo yasiende kombo
 • MWANGUZI
  mtu afanyaye kazi ya kuangusha matunda k.v-nazi kutoka kwenye mnazi
 • MWANAFASIHI
  mtu anayefanya kazi ya uandishi wa sanaa ya fasihi
 • MWANAMKENDE/KISABALUU/KIBERENGE/KAHABA/MALAYA/KIBIRITINGOMA/CHANGUDOA/MTALALESHI/MLUPO/GUBERI
  mwanamke anayefanya kazi ya kujiuza au kuuza mwili wake kwa wanaume kwa ajili ya kupata pesa
 • MNDEWA/JUMBE
  mtu ambaye ni kiongozi wa jamii yake,pia huitwa balozi wa kijiji
 • MWANAMICHEZO
  mtu ambaye kazi yake ni michezo,mdau wa michezo
 • MWANAMASUMBWI/MWANANDONDI
  anayefanya kazi ya kupigana ndondi au ngumi
 • MWANAMUZIKI/MWIMBAJI
  mtu anayefanya kazi ya kuimba kwa kutumia zana za muziki
 • MWANARIADHA
  anayefanya kazi ya mbio;riadha.mchezaji wa riadha
 • MWANARIWAYA
  anayefanya kazi ya kuandika vitabu vya hadithi,novela au riwaya
 • MWANASARUFU
 • mtu ambaye kazi yake hushughulikia taaluma ya sarufi
 • MWANASAYANSI
  mtu ambaye kazi yake inashughulikia uchunguzi,upimaji,majaribi
 • UTEDI
  mtumishi wa cheo kidogo afanyaye kazi katika chombo cha bahari k.v kukiosha na kuwapa watu chakula
 • MAMANTILIE
  mtu hasa wa kike anayeuza chakula magengeni au nyumbani
 • MAMLUKI
  huyu ni askari wa kukodiwa ili kupigana katika nchi jirani
 • HARAMIA
  huyu ni mnyang’anyi wa baharini.Gaidi wa baharini.
 • MAKANIKA
  fundi wa kutengeneza magari,mashine,Injini,Meli,pikipiki au mitambo ya vyuma(Chuma)
 • MANAMBA
  wafanyakazi wahamiaji katika mashamba makubwa
 • MCHINJAJI
  mtu anayefanya kazi ya kuchinja wanyama na kuwauza kwenye bucha
 • MCHORAJI
  mtu anayefanya kazi ya kuchora picha
 • LUGOJO
  watu wanaolinda kwa zamu
 • MFAGIZI/MFAGIAJI
  mtu anayefagia
 • MFARISHI
  mtu anayefanya kazi ya kutandika kitanda
 • MRINA
  fundi stadi wa kuvuna na kupakua asali
 • RUGARUGA
  mtu ambaye anafanya kazi chini ya amri ya chifu
 • KIBICHAMBO
  mtu hasa wa kike anayetumiwa kufanya kazi ya kunasa adui wa upande hasimu
 • FUNDIBOMBA
  mtu atengenezaye mifereji ya maji na kuunganisha paipu za mifereji na mitaro(PLUMBER)
 • MKWEZI
  anayepanda au kuaramia miti kv minazi na kuangua nazi
 • MFUANAZI
  mtu anayetoa makumbi kwenye nazi
 • KOSTEBO
  Afisa katika kikosi Cha usalama wa Umma kama vile Polisi,Jeshi nk asiye na cheo
 • MWALIMU/MDARISI/USTADH
  Mtu anayefundisha
 • NAHODHA
  mtu anayeendesha meli
 • SARAHANGI
  mtu anayemsaidia nahodha(nahodha wa pili)
 • KANDAWALA
  mtu anayeendesha garimoshi
 • DEREVA
  mtu anayeendesha gari
 • RUBANI
  mtu anayeendesha ndege
 • SAISI
  mtu anayefanya kazi ya kuchunga wanyama wanaopandwa kama vile Farasi,Punda,Ngamia n.k
 • MZEGAMZEGA
  mtu anayeuza maji kwa kuyatembeza
 • MGEMA
  mtu anayefanya kazi kukinga tembo la mnazi au kuchanja magome ili kupata utomvu au kutengeneza ulimbo
 • DALALI/MNADI
  mtu anayeuza bidhaa mnadani kwa kutangaza;**Zabuni-uza kwa kushindanisha bei
 • MACHINGA/MMACHINGA
  mtu anayefanya kazi ya biashara kwa kutembeza bidhaa zake aghalabu kwa miguu ili kuwatafuta wateja mf.’Malimali’
 • MCHUKUZI/HAMALI/MPAGAZI
  mtu anayefanya kazi ya kubeba mizigo kwa kutumia rukwama,toroli,bero/baro nk
 • MCHUUZI
  mtu afanyaye kazi ya biashara ya kuuza vitu rejareja mf.Hawker!
 • MKUNGA
  mtu anayewasaidia wanawake kukopoa au kujifungua
 • NGARIBA
  mtu anayetahiri vijana jandoni au unyagoni
 • MHASIBU
  Mtu anayefanya kazi ya kusimamia fedha katika kampuni,shule,chuo,Benki,Kikundi au chama
 • KESHIA
  Mtu anayepokea malipo na kuandikia wanaolipa stakabadhi au risiti ya malipo
 • MWANASAYANSI
  mtu ambaye kazi yake inashughulikia uchunguzi,ugunduzi,upimaji,majaribio na kuthibitishwa kwa muda uliopo
 • MWANASOKA
  mtu anayefanya kazi ya kucheza mpira wa miguu,soka,kabumbu,gozi au kandanda
 • MTAALAMU
  mtu anayefanya kazi taaluma aliyotaalamika ndani yake
 • MWANATAMTHILIA/MWANATAMTHILIYA
  mtu anayefanya kazi ya kuandika michezo ya kuigiza
 • MWANAHABARI/MTANGAZAJI
  mtu anayefanya kazi ya kutafuta,kuandika,kukusanya,kuhari na kutangaza au kusambaza taarifa au habari katika vyombo vya habari
 • MWANALEKSIKOLOGRAFIA
  mtu anayefanya kazi inayoshughulikia uchunguzi,uchambuzi na uchanganuzi wa msamiati wa lugha pamoja na maana yake
 • MLEHEMAJI
  mtu anayefanya kazi ya kuunganisha vitu hasa vyuma kwa kutumia madini aghalabu kwa kutumia risasi(WELDER)
 • MWANALEKSIKOGRAFIA
  mtu anayefanya kazi ya kuandika Kamusi
 • MSHAURINASAHA
 • mtu anayefanya kazi ya kutoa ushauri au nasaha kwa watu
 • MCHANGANUZI
  mtu afanyaye kazi ya kuchanganua masuala tofautitofauti.
 • MSWIRIZI
  Mtaalamu wa kufuga na kucheza na wanyama hayawani kama vile Nyoka,Nyani,Sokwe nk. (SNAKE CHARMER)
 • MHAKIKIMALI
  anayefanya kazi ya kuhakiki ubora wa bidhaa
 • MWAMIAJI/MWAMIZI
  afanyaye kazi ya kuamia ndege shamba
 • MWAMUZI
  anayesuluhisha ugomvi baina ya pande mbili au zaidi
 • REFA/MWAMUZI
  anayechezesha mchezo kulingana na sheria za mchezo husika
 • MWANAANGA
  afanyaye kazi ya utafiti wa mambo ya anga
 • MWANABAYOLOJIA
  mtaalamu wa masuala ya maisha na uhai wa viumbe na mimea
 • MWANADIPLOMASIA
  mtu anayefanya kazi kv katika ubalozi
 • MWANAGAINOKOLOJIA
  mtaalamu wa maradhi ya akina mama
 • MWANAISIMU
  mtaalamu wa masuala ya isimu na lugha
 • MWANAJESHI
  askari katika jeshi la ulinzi
 • MWANAMAJI/BAHARIA/MWANAPWA
  mtu anayefanya kazi katika chombo cha baharini
 • MWANASHERIA
  mtu utaalamu wa mambo ya sheria
 • MWANASIASA
  mtu anayejishughulisha na mambo ya siasa
 • MSHAIRI/MTUNZI/MALENGA
  mtu afanyaye kazi ya kutunga mashairi/nudhuma
 • MGHANI/MANJU
  gwiji katika kuimba mashairi
 • RAWI
  stadi katika kukariri au kusoma shairi bila kuimba
 • SHAHA
  mtu stadi katika kuhariri mashairi
 • MHARIRI
  stadi katika kusoma na kukosoa kazi ilioandikwa na mtu mwengine!
 • MNUNGURI/MKONOKONO
  mganga anayewatibu walioumwa na nyoka
 • MGIMBA
  mganga anayeaminika kuwezesha mvua kunyesha au kuizuia kimuujiza
 • MGAGAJI
  mtu anayefanya biashara ya kuwauzia watu bidhaa kwa bei za juu sana kidhuluma
 • MHAZIGI/MGANGAJI
  mtu mwenye ujuzi wa kutibu viungo vya mwili vilivyovunjika. Daktari wa mifupa na nyonga za mwili.
 • MGUNDUZI
  mtu anayefanya kazi ya kugundua na kudhihirisha kitu au jambo lililokuwa limejificha au lililokuwa halijulikani
 • SHUSHUSHU
  mtu anayepeleleza maisha ya watu kwa niaba ya serikali-afisa wa usalama wa taifa(SPY)
 • KUWADI/GAWADI/KIJUMBE/GAMBERA/MTALALESHI/KIBIRIKIZI
  mtu anayepeleleza habari za siri kutoka kwa mtu fulani kuenda kwa mwengine hasa kati ya mwanamke na mwanamume
 • MSASI/MRUMBA/MWINDAJI/MKAA
  mtu anayewinda wanyama msituni akiwa na idhini
 • KIJAKAZI/MJAKAZI/KISONOKO
  mtumwa mwanamke katika nyumba;mwanamke au msichana anayefanya kazi ya nyumba
 • JANGILI
  mtu anawinda wanyama katika mbuga za wanyama bila ya idhini ya serikali
 • JEMEDARI/AMIRI
  mkuu wa majeshi
 • JAMBAZI
  mtu anayefanya kazi ya wizi Kwa kuua akitumia Silaha hatari kama vile bunduki,Bastola nk.
 • MCHOPOZI/MCHOPOAJI
  mtu anayeiba kwa kutoa mfukoni au mkobani kwa kutumia vidole viwili kisirisiri
 • MNYANG’ANYI
  mtu anayeiba kwa kunyang’anya hadharani na guvu
 • SAJINI/SAJENTI
  askari mwenye cheo kilicho daraja moja zaidi kuliko koplo
 • KOPLO
  afisa wa jeshi au polisi aliye chini ya sajini na juu ya Konstebo-Mwandamizi
 • LUTENI
  ofisa wa kijeshi aliye chini ya kapteni na juu ya luteni usu
 • KAPTENI
  ofisa wa jeshi kati ya luteni na meja
 • MEJA
  ofisa wa jeshi mwenye cheo cha chini yd lutenikanali na juu ya kapteni
 • MEJAJENERALI
  ofisa wa jeshi aliye juu ya brigediajenerali na chini lutenijenerali
 • BRIGEDIA
  ofisa wa kijeshi mwenye cheo cha juu ya kanali na chini ya mejajenerali
 • LUTENI-JENERALI
  ofisa wa jeshi mwenye cheo cha juu ya meja-jenerali na chini ya jenerali
 • LUTENIKANALI
  ofisa wa jeshi mwenye cheo cha juu ya meja na chini ya kanali
 • KANALI
  ofisa wa jeshi aliye juu ya lutenikanali
 • LUTENIUSU
  ofisa wa cheo cha kwanza chini ya luteni
 • OFISAUGANI/AFISAUGANI
  ofisa mwenezi wa taarifa au maarifa fulani uwandani.
 • MHAKIKIMALI
  anayefanya kazi ya kuhakiki ubora wa bidhaa Kabla havijaenda sokoni Kwa mauzo
 • MWAMIAJI/MWAMIZI
  afanyaye kazi ya kuamia ndege kwenye shamba la vyakula
 • MSHAIRI/MTUNZI/MALENGA
  mtu afanyaye kazi ya kutunga mashairi/nudhuma
 • MGHANI/MANJU
  gwiji katika kuimba mashairi
 • RAWI
  stadi katika kukariri au kusoma shairi bila kuimba
 • SHAHA
  mtu stadi katika kuhariri mashairi
 • MHARIRI
  stadi katika kusoma na kukosoa kazi ilioandikwa na mtu mwengine!
 • KARII
  mtu anayesoma Kurani hasa Tajuwidi
 • KONDAKTA/TANIBOI/UTINGO/MAKANGA
  mtu anayepokea nauli kwenye gari pia hupakia na kupakua mizigo kwenye matwana,daladala au matatu
 • MSUKAJI
  mtu anayeshona,kutarizi au kufuma mkeka,jamvi,kanda au vikapu
 • BOSI/TAJIRI
  mkuu wa ofisi anayeajiri watu katika kazi
 • MRAMALI
  mtu anayetabiri mambo kwa kuvmia elimu ya nyota
 • MRATIBU
  mtu anayepanga,kuunganisha na kusimamia shughuli za watu mbalimbali katika kazi au ofisi
 • HATIBU
  mtu anayetoa hotuba kwa hadhira au hadhara(SpeechMaker.) **Mtu anayefanya kazi ya Kuzungumza Kwa Niaba ya kampuni,shirika, Serikali,chama,Kikundi au muungano(SPOKESPERSON)
 • BAYANA
  mtu stadi au fundi wa kusema,kuongea au kuhutubu kwa kutumia ujuzi wa lugha
 • MRASIMU
  mtu anayefanya kazi ya afisi na kulingana na taratibu na kanuni za utawala
 • WADENI
  Afisa mwenye dhamana ya kusimamia mahali k.v-mbuga za wanyama,hoteli,misitu,magereza(WARDEN/GAMEPAEK RANGER)
 • WAKALA/AJENTI
  mwakilishi wa kampuni,shirika au shughuli ya kibiashara
 • WARIA
  mtu aliye hodari katika kazi za mikono mf.ushonaji,uashi,uchongaji nk(ARTISAN)
 • UTEDI
  mtumishi wa cheo kidogo afanyaye kazi katika chombo cha bahari.
 • GADI/BAWABU/MLINZI/ASKARIGONGO
  Afisa wa usalama wa kibinafai anayefanya kazi ya Kulinda Uhai na Mali ya tajiri.
 • HADIMU
  Mtu anayefanya kazi ya kuwahhdumia wateja katika hoteli,mkahawa,mgahawa,dukani,supamaketi nk(WAITER)
 • NESI
  Mhudumu Afya anayewashughulikia wagonjwa katika hospitali au nyumbani.
 • MCHOPOZI/MCHOPOAJI
  mtu anayeiba kwa kutoa mfukoni au mkobani kwa kutumia vidole viwili kisirisiri
 • MNYANG’ANYI
  mtu anayeiba kwa kunyang’anya hadharani na guvu
 • SAJINI
  askari mwenye cheo kilicho daraja moja zaidi kuliko koplo
 • KOPLO
  afisa wa jeshi au polisi aliye chini ya sajini
 • LUTENI
  ofisa wa kijeshi aliye chini ya kapteni na juu ya luteni usu
 • KAPTENI
  ofisa wa jeshi kati ya luteni na meja
 • MEJA
  ofisa wa jeshi mwenye cheo cha chini yd lutenikanali na juu ya kapteni
 • MEJAJENERALI
  ofisa wa jeshi aliye juu ya brigediajenerali na chini lutenijenerali
 • BRIGEDIA
  ofisa wa kijeshi mwenye cheo cha juu ya kanali na chini ya mejajenerali
 • LUTENI-JENERALI
  ofisa wa jeshi mwenye cheo cha juu ya meja-jenerali na chini ya jenerali
 • LUTENIKANALI
  ofisa wa jeshi mwenye cheo cha juu ya meja na chini ya kanali
 • KANALI
  ofisa wa jeshi aliye juu ya lutenikanali
 • LUTENIUSU
  ofisa wa cheo cha kwanza chini ya luteni
 • OFISAUGANI/AFISAUGANI
  ofisa mwenezi wa taarifa au maarifa fulani uwandani

Print Friendly, PDF & Email
Tell your friends about this content:Leave a Reply 0